bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Revelation 9
Revelation 9
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 10 →
1
MALAIKA wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya inchi; akapewa ufunguo wa shimo la abuso.
2
Akalifungua shimo la abuso; moshi ukapanda kutoka lile shimo kama moshi wa tanuru kubwa: juu na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimo.
3
Nzige wakatoka katika lile shimo, wakaenda juu ya inchi, wakapewa nguvu kama nguvu za nge wa inchi.
4
Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya inchi wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, illa wale watu wasio ua muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.
5
Wakapewa amri wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na kuumwa kwao kulikuwa kama kuumwa na uge, aumapo mwana Adamu.
6
Na katika siku zile wana Adamu watatafuta mauti, nao hawataiona. Na watatamaui kufa, na mauti itawakimbia.
7
Na maumbo ya zile nzige kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao kama nyuso za wana Adamu.
8
Na walikuwa mi nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.
9
Na walikuwa na mabamba kifuani kama mabamba ya chuma. Na sauti ya mabawa yao kama sauti ya magari ya farasi wengi waendao kassi vitani.
10
Na wana mikia kama ya nge, na palikuwa kama viumo katika mikia yao. Na nguvu yao kuwadhuru wana Adamu miezi mitano.
11
Na juu yao wana mfalme, malaika wa abuso, jina lake kwa Kiebrania Abaddon, na kwa Kiyunani jina lake Apollion.
12
Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadae.
13
Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka mbele za Mungu,
14
ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue malaika wane waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrati.
15
Wale malaika wane wakafunguliwa, waliowekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka illi waue thuluth ya wana Adamu.
16
Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi elfu ishirini marra elfu kumi; nikasikia hesabu vao.
17
Ndivyo nilivyowaona farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana mabamba kifuani, ya moto, na ya samawati, na ya kiberiti; na vichwa vya farasi hawo kama vichwa vya simba, kukatoka katika vinywa vyao moto na moshi na kiberiti.
18
Thuluth ya wana Adamu wakauawa kwa matatu bayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho kilichotoka katika vinywa vyao.
19
Kwa maana nguvu zao ni katika vinywa vyao; maana mikia vao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, na kwa mikia hiyo wanadhuru.
20
Na wana Adamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia kazi za mikono yao hatta wasiwasujudu mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za mili, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.
21
Wala hawakutubia mauaji yao, wala uchawi wao, wala uasharati wao, wala kuiba kwao.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22