bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Titus 2
Titus 2
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
1
BALI wewe nena mambo yapasayo mafundisho ya uzima,
2
ya kama wazee wawe wenye kujimudu nafsi zao, wenye adahu, wenye kiasi, wazima katika imani na katika upendo na katika uvumilivu.
3
Na wazee wa kike vivyo hivyo wawe na mwenendo wa utakatifu, wasiwe wasiugiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;
4
illi wawatie akili wanawake vijana wawapende wanme zao, ka kuwapenda watoto wao,
5
na kuwa wenye niasi, na kuwa safi, kukaa nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao weuyewe, illi neno la Muugu lisitukanwe.
6
Na vijana vivyo hivyo nwaonye kuwa na kiasi;
7
katika mambo yote ukijionyesha kuwa namna ya matendo mema, katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahifu,
8
na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa, illi yule mwenye kupingana nawe ataliayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
9
Watumwa wawatii Bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu,
10
wasiwe waibaji, bali wakionyesha uaminifu mwema wote, illi wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu katika mambo yote.
11
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wana Adamu wote imeonekana;
12
yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ua kuishi kwa kiasi, na haki, na utawa, katika ulimwengu wa sasa,
13
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;
14
aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.
15
Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3