Hosea 14:10 — Compare Translations

3 translations compared side by side

Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeyote aliye na hekima ayaelewe mambo haya, mtu aliye na busara ayatambue. Maana njia za Mwenyezi-Mungu ni nyofu; watu wanyofu huzifuata, lakini wakosefu hujikwaa humo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuko nani aliye mwerevu wa kweli, ayatambue hayo? Yuko nani aliye mtambuzi, ayajue maana yao hayo? Kwani njia za Bwana hunyoka, nao waongofu huzishika, lakini wapotovu hukwazwa nazo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeyote anayekuwa na hekima aelewe mambo haya, mutu anayekuwa na akili ayatambue. Maana njia za Yawe ni zenye kunyooka; watu wa haki wanazifuata, lakini wenye zambi wanaanguka katika njia hizo.