bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Song of Solomon 2
Song of Solomon 2
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 3 →
1
Mimi ni ua la Sharoni, ni yungiyungi ya bondeni.
2
Kama yungiyungi kati ya michongoma, ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wasichana.
3
Kama mtofaa kati ya miti ya msituni, ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wavulana. Nafurahia kuketi chini ya kivuli chake, na tunda lake tamu sana kwangu.
4
Alinichukua hadi ukumbi wa karamu, akatweka bendera ya mapenzi juu yangu.
5
Nishibishe na zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, maana naugua kwa mapenzi!
6
Mkono wake wa kushoto chini ya kichwa changu, mkono wake wa kulia wanikumbatia.
7
Nawasihi enyi wanawake wa Yerusalemu, kama walivyo paa au swala wa porini, msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi, hadi hapo wakati wake utakapofika.
8
Hiyo ni sauti ya mpenzi wangu, yuaja mbio, anaruka milima, vilima anavipita kasi!
9
Mpenzi wangu ni kama paa, ni kama swala mchanga. Amesimama karibu na ukuta wetu, achungulia dirishani, atazama kimiani.
10
Mpenzi wangu aniambia: “Inuka basi, ewe mpenzi wangu, unipendezaye, njoo twende zetu.
11
Tazama, majira ya baridi yamepita, nazo mvua zimekwisha koma;
12
maua yamechanua kila mahali. Wakati wa kuimba umefika; sauti ya hua yasikika mashambani mwetu.
13
Mitini imeanza kuzaa; na mizabibu imechanua; inatoa harufu nzuri. Njoo, basi, ewe mpenzi wangu unipendezaye, njoo twende.
14
Ee hua wangu, uliyejificha miambani. Hebu niuone uso wako, hebu niisikie sauti yako, maana sauti yako yapendeza na uso wako wavutia.
15
“Tukamatieni mbweha, wale mbweha wadogowadogo, wanaoiharibu mizabibu yetu inayochanua.”
16
Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake. Yeye hulisha kondoo wake penye yungiyungi,
17
hadi hapo jua linapochomoza na vivuli kutoweka. Rudi kama paa mpenzi wangu, kama swala mdogo juu ya milima ya Betheri.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8