bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Song of Solomon 8
Song of Solomon 8
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
1
Laiti ungekuwa kaka yangu, ambaye amenyonyeshwa na mama yangu! Hivyo, hata kama ningekutana nawe nje, ningekubusu na hakuna ambaye angenidharau.
2
Ningekuongoza na kukufikisha nyumbani kwa mama mzazi, mahali ambapo ungenifundisha upendo. Ningekupa divai nzuri iliyokolezwa, ningekupa divai yangu ya makomamanga yangu.
3
Mkono wako wa kushoto u chini ya kichwa changu, na mkono wako wa kulia wanikumbatia.
4
Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu, msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi, hadi hapo wakati wake utakapofika.
5
Ni nani huyu ajaye kutoka mbugani, huku anamwegemea mpenzi wake? Chini ya mtofaa, mimi nilikuamsha, pale ambapo mama yako aliona uchungu, naam, pale ambapo mama yako alikuzaa.
6
Nipige kama mhuri moyoni mwako, naam, kama mhuri mikononi mwako. Maana pendo lina nguvu kama kifo, wivu nao ni mkatili kama kaburi. Mlipuko wake ni kama mlipuko wa moto, huwaka kama mwali wa moto.
7
Maji mengi hayawezi kamwe kulizima, mafuriko hayawezi kulizamisha. Mtu akijaribu kununua pendo, akalitolea mali yake yote, atakachopata ni dharau tupu.
8
Tunaye dada mdogo, ambaye bado hajaota matiti. Je, tumfanyie nini dada yetu siku atakapoposwa?
9
Kama angalikuwa ukuta, tungalimjengea mnara wa fedha; na kama angalikuwa mlango, tungalimhifadhi kwa mbao za mierezi.
10
Mimi nalikuwa ukuta, na matiti yangu kama minara yake. Machoni pake nalikuwa kama mwenye kuleta amani.
11
Solomoni alikuwa ana shamba la mizabibu, mahali paitwapo Baal-hamoni. Alilikodisha kwa walinzi; kila mmoja wao alilipa vipande elfu vya fedha.
12
Shamba langu la mizabibu ni shamba langu mwenyewe, naam, ni shamba langu binafsi! Basi, Solomoni, wewe ukae na elfu zako za fedha, na kila mlinzi wa matunda akae na mia mbili zake.
13
Ewe uliye shambani, rafiki zangu wanasikiliza sauti yako; hebu nami niisikie tafadhali!
14
Njoo haraka ewe mpenzi wangu, kama paa au mwanapaa dume juu ya milima ya manukato.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8