bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
1 Chronicles 18
1 Chronicles 18
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 19 →
1
Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, akautwaa Gathi pamoja na vijiji vinavyouzunguka kutoka katika utawala wa Wafilisti.
2
Daudi akawashinda pia Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru.
3
Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alipokwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Eufrati.
4
Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.
5
Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao.
6
Kisha Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumishi wa Daudi, wakawa wanamletea ushuru. BWANA akampa Daudi ushindi kila mahali alipokwenda.
7
Daudi akatwaa zile ngao za dhahabu zilizochukuliwa na maafisa wa Hadadezeri, akazileta Yerusalemu.
8
Kutoka mji wa Tibhathi na mji wa Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akachukua pia shaba nyingi sana, ambayo Solomoni aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.
9
Tou mfalme wa Hamathi aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri mfalme wa Soba,
10
akamtuma mwanawe, Hadoramu kwa Mfalme Daudi ili kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake juu ya Mfalme Hadadezeri vitani, kwa kuwa alikuwa amepigana vita mara nyingi na Tou. Hadoramu akamletea Daudi vifaa mbalimbali vya dhahabu fedha na shaba.
11
Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa BWANA kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki.
12
Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.
13
Akaweka askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. BWANA akampa Daudi ushindi kila mahali alipokwenda.
14
Daudi akatawala katika Israeli yote, akitenda lililo haki na lililo sawa kwa watu wake wote.
15
Yoabu, mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa jeshi, Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mtunza kumbukumbu,
16
Sadoki, mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, Shavsha alikuwa mwandishi,
17
naye Benaya, mwana wa Yehoyada alisimamia Wakerethi na Wapelethi, nao wana wa Daudi walikuwa maafisa wakuu katika utumishi wa mfalme.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29