bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Job 24
Job 24
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 25 →
1
“Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio?
2
Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyang'anya kwa nguvu.
3
Huwanyang'anya yatima punda wao na kumchukua rehani fahali wa mjane.
4
Humsukuma mhitaji kutoka katika njia na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha.
5
Kama punda-mwitu jangwani, maskini huzunguka katika kazi zao wakitafuta chakula; mahali pasipokaliwa na watu wala kulimika hupata chakula cha watoto wao.
6
Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo katika mashamba ya mizabibu ya waovu.
7
Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa bila nguo, hawana cho chote cha kujifunika baridi.
8
Hutota kwa mvua za mlimani, nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri.
9
Watoto wasio na baba hupokonywa matitini; watoto wachanga wa maskini hukamatwa kwa nguvu kwa ajili ya deni.
10
Kwa kukosa nguo, hutembea uchi; hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa.
11
Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia, hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu.
12
Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. Lakini Mungu hamlaumu mtu ye yote kwa kutenda mabaya.
13
“Wako wale wanaoiasi nuru, wasiofahamu njia zake wala hawakai katika mapito yake.
14
Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, mwuaji huinuka naye huwaua maskini na mhitaji, wakati wa usiku huiba kama mwivi.
15
Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza, naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’ naye huuficha uso wake.
16
Katika giza, huvunja majumba, lakini wakati wa mchana hujifungia ndani, hawataki kufanya lo lote nuruni.
17
Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao, hujifanya rafiki na vitisho vya gizani.
18
“Lakini wao ni povu juu ya maji; sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa, hivyo hakuna hata mmoja aendaye kwenye shamba la mizabibu.
19
Kama vile joto na hari vikaushavyo theluji iliyoyeyuka, ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo wale waliotenda dhambi.
20
Tumbo lililowazaa huwasahau, nao huwa karamu ya mabuu; watu waovu hawakumbukwi tena, lakini huvunjika kama mti.
21
Huwafanya mawindo wanawake walio tasa na wale wasio na watoto, nao hawaonyeshi huruma kwa wajane.
22
Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake, ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha.
23
Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, lakini macho yake yanaona njia zao.
24
Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka, hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, hukatwa kama masuke ya nafaka.
25
“Kama hili sivyo, ni nani awezaye kuthibitisha kuwa mimi ni mwongo na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?”
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42