bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Job 38
Job 38
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 39 →
1
Kisha BWANA akamjibu Ayubu kutoka katika upepo wa kisulisuli. Akasema:
2
“Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa?
3
Jikaze kama mwanaume, nami nitakuuliza swali, nawe unijibu.
4
“Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu.
5
Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? Hakika wewe unajua! Ni nani aliyenyosha kamba ya kupimia juu yake?
6
Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,
7
wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?
8
“Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka katika tumbo,
9
nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake na kuyafungia katika giza nene,
10
Nilipoamuru mipaka yake na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,
11
niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi, hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?
12
“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,
13
yapate kushika miisho ya dunia na kuwakung'uta waovu waliomo?
14
Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri; sura yake hukaa kama ile ya vazi.
15
Waovu huzuiliwa nuru yao, nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.
16
“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?
17
Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti? Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti?
18
Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote.
19
“Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako masikani mwagiza ni wapi?
20
Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake? Unajua njia za kufika maskani mwake?
21
Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa! Kwani umeishi miaka mingi!
22
“Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji au kuona ghala za mvua ya mawe,
23
ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu, na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano?
24
Ipi ni njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa, au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia?
25
Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi na njia ya umeme wa radi,
26
ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu, jangwa lisilo na ye yote ndani yake,
27
ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa na majani yaanze kumea ndani yake?
28
Je, mvua ina baba? Ni nani baba azaaye matone ya umande?
29
Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Ni nani aliyezaa ukungu kutoka mbinguni
30
wakati maji yawapo magumu kama jiwe, wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda?
31
“Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia? Waweza kulegeza kamba za Orioni?
32
Waweza kuliongoza kundi la nyota kwa majira yake au kuongoza Dubu na watoto wake?
33
Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?
34
“Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji?
35
Wewe je, hutuma umeme wa radi kwenye njia zake? Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’?
36
Ni nani aliyeujalia moyo hekima au kuzipa akili ufahamu?
37
Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni
38
wakati mavumbi yawapo magumu na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?
39
“Je, utamwindia simba jike mawindo na kuwashibisha simba wenye njaa
40
wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao au wakivizia kichakani?
41
Ni nani ampaye kunguru chakula wakati makinda yake yanapomlilia Mungu yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 39 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42