bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Leviticus 23
Leviticus 23
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 24 →
1
BWANA akamwambia Mose,
2
“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Hizi ndizo sikukuu zangu zilizoamuriwa, sikukuu zilizoamuriwa za BWANA, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu.
3
“ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yo yote, po pote mnapoishi, ni Sabato kwa BWANA.
4
“ ‘Hizi ni sikukuu za BWANA zilizoamuriwa, makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilizoamuriwa:
5
Pasaka ya BWANA huanza jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
6
Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa kwanza Sikukuu ya BWANA ya Mikate Isiyotiwa Chachu huanza; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu.
7
Katika siku ya kwanza mtafanya kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.
8
Kwa siku saba mtamletea BWANA sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku hiyo ya saba mtafanya kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.’ ”
9
BWANA akamwambia Mose,
10
“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi nitakayowapa na kuvuna mazao ya nchi hiyo, leteni kwa kuhani mganda wa mavuno ya kwanza ya nafaka.
11
Naye atauinua huo mganda mbele za BWANA ili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato.
12
Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwa BWANA dhabihu ya kuteketezwa kwa moto mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari,
13
pamoja na sadaka ya unga laini wa nafaka sehemu mbili za kumi za efa uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka ya kinywaji robo ya hini ya divai.
14
Kamwe msile mkate wo wote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, mpaka siku ile mtakayomletea Mungu wako sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo po pote mnapoishi.
15
“ ‘Tangu siku ile iliyofuata Sabato, siku mliyotoa sadaka ya mganda wa kuinuliwa, hesabuni majuma saba kamili.
16
Mtahesabu mpaka siku inayofuata Sabato ya saba, siku hamsini, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwa BWANA.
17
Kutoka po pote mnapoishi, leteni mikate miwili iliyookwa kwa unga laini, sehemu mbili za kumi za efa uliookwa wenye chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwa BWANA.
18
Toeni pamoja na hiyo mikate wana-kondoo saba, kila mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, fahali mchanga, na kondoo waume wawili. Watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwa BWANA, pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, sadaka iliyotolewa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
19
Kisha toeni dhabihu mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili kila mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya amani.
20
Kuhani atawainua hao wana-kondoo wawili mbele za BWANA kuwa sadaka ya kuinuliwa, pamoja na mkate wa malimbuko. Ni sadaka takatifu kwa BWANA kwa ajili ya kuhani.
21
Siku iyo hiyo mtatangaza kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo po pote mnapoishi.
22
“ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.’ ”
23
BWANA akamwambia Mose,
24
“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu kwa ukumbusho pamoja na kupigwa kwa tarumbeta.
25
Msifanye kazi zenu zo zote za kawaida, lakini toeni sadaka kwa BWANA iliyoteketezwa kwa moto.’ ”
26
BWANA akamwambia Mose,
27
“Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, nanyi mtoe sadaka kwa BWANA ya kuteketezwa kwa moto.
28
Msifanye kazi siku hiyo, kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, upatanisho unapofanyika kwa ajili yenu mbele za BWANA Mungu wenu.
29
Mtu ye yote ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
30
Mtu ye yote atakayefanya kazi siku hiyo nitamwangamiza kutoka miongoni mwa watu wake.
31
Hamtafanya kazi kamwe. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo po pote mnapoishi.
32
Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, ni lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”
33
BWANA akamwambia Mose,
34
“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu ya BWANA ya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba.
35
Siku ya kwanza ni kusanyiko takatifu, msifanye kazi zenu za kawaida.
36
Kwa siku saba toeni sadaka kwa BWANA za kuteketezwa kwa moto, kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu na mtoe sadaka kwa BWANA ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.
37
(“ ‘Hizi ni sikukuu za BWANA zilizoamuriwa, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu kwa kuleta sadaka kwa BWANA za kuteketeza kwa moto: sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, dhabihu na sadaka za vinywaji zitahitajika kila siku.
38
Sadaka hizi ni nyongeza ya zile mnazozitoa katika Sabato za BWANA, na pia ni nyongeza ya matoleo yenu ya cho chote mlichoweka nadhiri, na sadaka zenu zote za hiari mnazozitoa kwa BWANA.)
39
“ ‘Basi kuanzia siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, baada ya kuvuna mazao yote ya nchi, mtaadhimisha sikukuu kwa BWANA kwa siku saba; siku ya kwanza ni mapumziko, pia siku ya nane ni mapumziko.
40
Kwenye siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele za BWANA Mungu wenu kwa siku saba.
41
Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwa BWANA kwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni kwenye mwezi wa saba.
42
Mtaishi katika vibanda kwa siku saba: Wazawa wote wa Waisraeli wataishi katika vibanda,
43
ili wazao wenu wajue kuwa niliwafanya Waisraeli waishi kwenye vibanda nilipowatoa Misri. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.’ ”
44
Kwa hiyo Mose akawatangazia Waisraeli sikukuu zilizoamuriwa na BWANA.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27