bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Leviticus 24
Leviticus 24
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 25 →
1
BWANA akamwambia Mose,
2
“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi yaliyokamuliwa ya zeituni kwa ajili ya mwanga ili kwamba taa ziwe zinawaka mfululizo.
3
Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za BWANA kuanzia jioni hadi asubuhi kwa mfululizo. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
4
Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za BWANA lazima zihudumiwe mfululizo.
5
“Chukua unga laini na uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa za unga kwa kila mkate.
6
Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za BWANA juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi.
7
Kando ya kila mstari weka uvumba safi kama sehemu ya ukumbusho ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa kuteketezwa kwa moto.
8
Mikate hii itawekwa mbele za BWANA kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu.
9
Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa kuteketezwa kwa moto.”
10
Basi mwana wa mama wa Kiisraeli ambaye baba yake ni Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli na mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.
11
Huyu mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru Jina la BWANA na kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri wa kabila la Dani.)
12
Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya BWANA yatakapokuwa wazi kwao.
13
Ndipo BWANA akamwambia Mose:
14
“Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe.
15
Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu ye yote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake;
16
ye yote atakayekufuru Jina la BWANA ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwapo ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la BWANA, ni lazima auawe.
17
“ ‘Kama mtu ye yote atamwua mtu mwingine, ni lazima auawe.
18
Mtu ye yote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai.
19
Ikiwa mtu ye yote atamjeruhi jirani yake, cho chote alichomtenda naye atatendewa:
20
iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa.
21
Ye yote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini ye yote auaye mtu, lazima auawe.
22
Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.’ ”
23
Kisha Mose akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Mose.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27