bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
1 Chronicles 23
1 Chronicles 23
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 24 →
1
Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Sulemani mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.
2
Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.
3
Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000.
4
Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi,
5
na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”
6
Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
7
Wana wa Wagershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei.
8
Wana wa Ladani walikuwa watatu: Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.
9
Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomothi, Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.
10
Nao wana wa Shimei walikuwa wanne: Yahathi, Zina, Yeushi na Beria.
11
Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.
12
Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
13
Wana wa Amramu walikuwa: Haruni na Musa. Haruni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la bwana milele.
14
Wana wa Musa mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.
15
Wana wa Musa walikuwa: Gershomu na Eliezeri.
16
Wazao wa Gershomu: Shebueli alikuwa wa kwanza.
17
Wazao wa Eliezeri: Rehabia alikuwa wa kwanza. Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
18
Wana wa Ishari: Shelomithi alikuwa wa kwanza.
19
Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.
20
Wana wa Uzieli walikuwa: Mika wa kwanza na Ishia wa pili.
21
Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Wana wa Mahli walikuwa: Eleazari na Kishi.
22
Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23
Wana wa Mushi: Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.
24
Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la bwana.
25
Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele,
26
Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.”
27
Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.
28
Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Haruni kuhudumu katika Hekalu la bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.
29
Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa.
30
Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu bwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni
31
na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.
32
Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Haruni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la bwana.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29