bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
1 Thessalonians 1
1 Thessalonians 1
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
1
Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kundi la waumini la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu, na ndani ya Bwana Isa Al-Masihi: Neema iwe kwenu na amani.
2
Siku zote tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima.
3
Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Isa Al-Masihi.
4
Ndugu zetu mpendwao na Mungu, kwa kuwa tunajua kwamba Mungu amewachagua,
5
kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho wa Mwenyezi Mungu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu.
6
Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana Isa, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho wa Mwenyezi Mungu.
7
Hivyo ninyi mkawa kielelezo kwa waumini wote katika Makedonia na Akaya.
8
Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana Isa limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mwenyezi Mungu imejulikana kila mahali kiasi kwamba hatuna haja ya kusema lolote kwa habari yake.
9
Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mwenyezi Mungu aliye hai na wa kweli,
10
na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mwenyezi Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani, Isa, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5