bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
1 Thessalonians 4
1 Thessalonians 4
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
1
Hatimaye, ndugu, tuliwaomba na kuwasihi katika Bwana Isa kwamba, kama mlivyojifunza kutoka kwetu jinsi iwapasavyo kuishi ili kumpendeza Mwenyezi Mungu, kama vile mnavyoishi, imewapasa mzidi sana kufanya hivyo.
2
Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Isa.
3
Mapenzi ya Mwenyezi Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa,
4
ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima,
5
si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mwenyezi Mungu.
6
Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali.
7
Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu.
8
Kwa hiyo, mtu yeyote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mwenyezi Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
9
Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mwenyezi Mungu kupendana.
10
Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda.
11
Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza,
12
ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote.
13
Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini.
14
Kwa kuwa tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka, na kwa hivyo, Mwenyezi Mungu kwa njia ya Isa atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini ndani yake.
15
Kulingana na neno la Bwana Isa mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana Isa, hakika hatutawatangulia waliolala mauti.
16
Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza.
17
Baada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana Isa hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana Isa milele.
18
Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5