bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Deuteronomy 16
Deuteronomy 16
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 17 →
1
Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya bwana Mwenyezi Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.
2
Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ng’ombe, mahali pale ambapo bwana atapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.
3
Msile nyama hiyo pamoja na mikate iliyotiwa chachu, lakini kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, mikate ya kujitesa, kwa sababu mliondoka Misri kwa haraka, ili kwamba siku zote za maisha yenu mpate kukumbuka wakati wenu wa kuondoka Misri.
4
Chachu isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yoyote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.
5
Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wowote ambao bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa,
6
isipokuwa mahali atakapopachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. Hapo ndipo lazima mtoe dhabihu ya Pasaka jioni, jua litakapotua, iwe kumbukumbu yenu ya kutoka Misri.
7
Okeni na mle mahali pale ambapo bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapopachagua, kisha asubuhi mrudi kwenye mahema yenu.
8
Kwa siku sita mtakula mikate isiyotiwa chachu na siku ya saba fanyeni kusanyiko kwa ajili ya bwana Mwenyezi Mungu wenu na msifanye kazi.
9
Mhesabu majuma saba tangu wakati mnapoanza kuchukua mundu kuvuna nafaka.
10
Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa.
11
Shangilieni mbele za bwana Mwenyezi Mungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu.
12
Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa kule Misri na mfuate amri hizi kwa uangalifu.
13
Adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa siku saba baada ya kukusanya mazao yenu ya nafaka na kukamua zabibu.
14
Mfurahie sikukuu yenu, ninyi, wana wenu, binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu.
15
Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya bwana Mwenyezi Mungu wenu katika mahali atakapopachagua bwana. Kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.
16
Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele za bwana Mwenyezi Mungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele za bwana mikono mitupu:
17
Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyo bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyowabariki.
18
Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambao bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa.
19
Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki.
20
Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa.
21
Msisimamishe nguzo yoyote ya Ashera kando ya madhabahu mliyomjengea bwana Mwenyezi Mungu wenu,
22
wala msisimamishe jiwe la kuabudu, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu wenu anavichukia vitu hivi.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34