bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Deuteronomy 5
Deuteronomy 5
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 6 →
1
Musa akawaita Israeli wote, akawaambia: Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata.
2
bwana Mwenyezi Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu.
3
Si kwamba bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo.
4
bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima.
5
(Wakati huo nilisimama kati ya bwana na ninyi kuwatangazia neno la bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:
6
“Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
7
Usiwe na miungu mingine ila mimi.
8
Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji.
9
Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, bwana Mwenyezi Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
10
lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
11
Usilitaje bure jina la bwana Mwenyezi Mungu wako, kwa kuwa bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
12
Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokuagiza.
13
Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote.
14
Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa bwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ng’ombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe.
15
Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo bwana Mwenyezi Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.
16
Waheshimu baba yako na mama yako, kama bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi bwana Mwenyezi Mungu wako anayokupa.
17
Usiue.
18
Usizini.
19
Usiibe.
20
Usimshuhudie jirani yako uongo.
21
Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ng’ombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”
22
Hizi ndizo amri alizozitangaza bwana kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.
23
Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi.
24
Nanyi mkasema, “ bwana Mwenyezi Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye.
25
Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya bwana Mwenyezi Mungu wetu zaidi.
26
Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi?
27
Sogea karibu usikie yale yote asemayo bwana Mwenyezi Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho bwana Mwenyezi Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”
28
bwana aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na bwana akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri.
29
Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!
30
“Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao.
31
Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”
32
Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.
33
Fuateni yale yote ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34