bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
John 11
John 11
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 12 →
1
Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania kijiji cha Maria na Martha dada zake.
2
Huyu Maria, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye yule ambaye alimpaka Bwana Isa mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake.
3
Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Isa kumwambia, “Bwana Isa, yule umpendaye ni mgonjwa.”
4
Lakini Isa aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.”
5
Pamoja na hivyo, ingawa Isa aliwapenda Martha, Maria na Lazaro ndugu yao,
6
baada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi.
7
Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Haya, turudi Uyahudi.”
8
Wanafunzi wake wakamwambia, “Mwalimu, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?”
9
Isa akawajibu, “Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wala watembeao mchana hawawezi kujikwaa kwa maana wanaona nuru ya ulimwengu huu.
10
Lakini wale watembeao usiku hujikwaa kwa sababu hakuna nuru ndani yao.”
11
Baada ya kusema haya, Isa akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha.”
12
Wanafunzi wakamwambia, “Bwana Isa, kama amelala usingizi ataamka.”
13
Hata hivyo, Isa alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu.
14
Kwa hiyo Isa akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa.
15
Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwepo huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake.”
16
Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye.”
17
Isa alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne.
18
Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu umbali wa karibu maili mbili,
19
nao Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Maria kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao.
20
Martha aliposikia kwamba Isa anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Maria alibaki nyumbani.
21
Martha akamwambia Isa, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.
22
Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.”
23
Isa akamwambia, “Ndugu yako atafufuka.”
24
Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.”
25
Isa akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi
26
na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?”
27
Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.”
28
Baada ya kusema haya Martha alikwenda, akamwita Maria dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.”
29
Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Isa.
30
Isa alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha.
31
Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko.
32
Maria alipofika mahali pale Isa alipokuwa, alipiga magoti miguuni pake na kusema, “Bwana Isa, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.”
33
Isa alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Isa alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana.
34
Akauliza, “Mmemweka wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo upaone.”
35
Isa akalia machozi.
36
Ndipo Wayahudi wakasema, “Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!”
37
Lakini wengine wakasema, “Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”
38
Isa kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake.
39
Isa akasema, “Liondoeni hilo jiwe.” Martha, ndugu yake yule aliyekuwa amekufa, akasema, “Lakini Bwana Isa, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwa kaburini siku nne.”
40
Isa akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”
41
Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka kaburini. Isa akainua macho yake juu, akasema, “Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia.
42
Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya umati huu uliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.”
43
Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, “Lazaro, njoo huku!”
44
Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Isa akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”
45
Hivyo Wayahudi wengi waliokuwa wamekuja kumfariji Maria, walipoona yale Isa aliyoyatenda wakamwamini.
46
Lakini baadhi yao wakaenda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo Isa aliyoyafanya.
47
Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza. Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi.
48
Kama tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.”
49
Mmoja wao aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, akasema, “Ninyi hamjui kitu chochote!
50
Hamjui kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote liangamie?”
51
Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Isa angelikufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi,
52
wala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja.
53
Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Isa.
54
Kwa hiyo Isa akawa hatembei hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake.
55
Basi Pasaka ya Wayahudi ilipokuwa imekaribia, watu wengi walitoka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajitakase.
56
Watu wakawa wanamtafuta Isa, nao waliposimama kwenye eneo la Hekalu waliulizana, Je, mtu huyu hatakuja kamwe kwenye Sikukuu?
57
Viongozi wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa yeyote atakayejua mahali Isa aliko, lazima atoe taarifa ili wapate kumkamata.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21