bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
John 12
John 12
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 13 →
1
Siku sita kabla ya Pasaka, Isa alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Isa alikuwa anaishi.
2
Wakaandaa karamu kwa heshima ya Isa. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Isa.
3
Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.
4
Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Isa, akasema,
5
“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300 na fedha hizo wakapewa maskini?”
6
Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.
7
Isa akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
8
Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”
9
Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Isa alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Isa, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Isa alikuwa amemfufua.
10
Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia,
11
kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Isa na kumwamini.
12
Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Isa angekuja Yerusalemu.
13
Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana Mwenyezi Mungu!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
14
Isa akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,
15
“Usiogope, Ewe binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda!”
16
Wanafunzi wake Isa mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Isa alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.
17
Wale waliokuwepo wakati Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia.
18
Ni kwa sababu pia walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu ndiyo maana umati wa watu ukaenda kumlaki.
19
Hivyo Mafarisayo walipoona hayo, wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”
20
Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu.
21
Hawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Isa.”
22
Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Isa.
23
Isa akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
24
Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi.
25
Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele.
26
Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.
27
“Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii.’ Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.
28
Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”
29
Ule umati wa watu uliokuwa mahali pale uliisikia nao ukasema, “Hiyo ni sauti ya radi,” wengine wakasema, “Malaika ameongea naye.”
30
Isa akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu.
31
Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.
32
Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.”
33
Isa aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa.
34
Ule umati wa watu ukapiga kelele, ukasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba ‘Al-Masihi adumu milele.’ Wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu?’ Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”
35
Ndipo Isa akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakokwenda.
36
Wekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Isa aliondoka, akajificha wasimwone.
37
Hata baada ya Isa kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini.
38
Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Bwana Mwenyezi Mungu, ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Bwana Mwenyezi umefunuliwa kwa nani?”
39
Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine:
40
“Amewafanya vipofu, na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka nami nikawaponya.”
41
Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Isa na kunena habari zake.
42
Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi.
43
Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
44
Isa akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma.
45
Yeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma.
46
Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.
47
“Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa.
48
Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
49
Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema.
50
Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21