bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Numbers 16
Numbers 16
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 17 →
1
Kora mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, pamoja na baadhi ya Wareubeni, yaani Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni mwana wa Pelethi, wakachukua baadhi ya watu,
2
wakainuka dhidi ya Musa. Pamoja nao walikuwepo wanaume wa Kiisraeli 250, watu waliojulikana, viongozi wa jumuiya waliokuwa wameteuliwa kuwa wakuu wa kusanyiko.
3
Wakaja kama kikundi kuwapinga Musa na Haruni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili lote ni takatifu, kila mmoja wao, naye bwana yu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko la bwana?”
4
Musa aliposikia jambo hili, akaanguka kifudifudi.
5
Kisha akamwambia Kora na wafuasi wake wote: “Asubuhi bwana ataonyesha ni nani aliye wake na ni nani aliye mtakatifu, tena atamtaka mtu huyo aje kwake. Mtu yule ambaye atamchagua atamfanya kuja karibu naye.
6
Wewe Kora na wafuasi wako wote mtafanya hivi: Chukueni vyetezo,
7
kesho wekeni moto na uvumba kwenye hivyo vyetezo mbele za bwana. Mtu ambaye bwana atamchagua atakuwa ndiye mtakatifu. Ninyi Walawi mmejitukuza sana!”
8
Pia Musa akamwambia Kora, “Enyi Walawi! Sasa nisikilizeni.
9
Haiwatoshi ninyi kwamba Mungu wa Israeli amewateua ninyi kutoka kusanyiko lote la Kiisraeli, na kuwaleta karibu naye mpate kufanya kazi kwenye Maskani ya bwana, na kusimama mbele ya kusanyiko ili kuwahudumia?
10
Amekuleta wewe na ndugu zako Walawi mwe karibu naye, lakini sasa unajaribu kupata na ukuhani pia.
11
Wewe na wafuasi wako wote mmekusanyika pamoja kinyume cha bwana. Haruni ni nani kwamba ninyi mnung’unike dhidi yake?”
12
Kisha Musa akawaita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu. Lakini wao wakasema, “Sisi hatuji!
13
Haitoshi tu kwamba wewe umetuleta kutoka nchi itiririkayo maziwa na asali ili kutuua sisi jangwani? Nawe sasa pia unataka kuwa mkuu juu yetu?
14
Zaidi ya hayo, hujatuingiza katika nchi inayotiririka maziwa na asali, wala hujatupa urithi wa mashamba na mashamba ya mizabibu. Je, utayang’oa macho ya watu hawa? Hapana, sisi hatuji!”
15
Ndipo Musa akakasirika sana na kumwambia bwana, “Usiikubali sadaka yao. Mimi sikuchukua chochote, hata punda kutoka kwao, wala sijamkosea hata mmoja wao.”
16
Musa akamwambia Kora, “Wewe na wafuasi wako wote kesho mtatokea mbele za bwana: yaani wewe na hao wenzako, pamoja na Haruni.
17
Kila mtu atachukua chetezo chake na kuweka uvumba ndani yake, vyetezo 250 kwa jumla, na kukileta mbele za bwana. Wewe na Haruni mtaleta vyetezo vyenu pia.”
18
Kwa hiyo kila mtu akachukua chetezo chake, akaweka moto na uvumba ndani yake, na kusimama pamoja na Musa na Haruni kwenye mlango wa Hema la Kukutania.
19
Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Musa na Haruni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa bwana ukatokea kwa kusanyiko lote.
20
bwana akamwambia Musa na Haruni,
21
“Jitengeni kutoka kwenye kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”
22
Lakini Musa na Haruni wakaanguka kufudifudi na kulia kwa sauti, wakasema, “Ee Mungu, Mungu wa roho za wanadamu wote, utakuwa na hasira na kusanyiko lote wakati ni mtu mmoja tu ametenda dhambi?”
23
Ndipo bwana akamwambia Musa,
24
“Liambie kusanyiko, ‘Ondokeni hapo karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu.’ ”
25
Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu, nao wazee wa Israeli wakafuatana naye.
26
Musa akalionya kusanyiko, “Sogeeni nyuma mbali na mahema ya hawa watu waovu! Msiguse kitu chochote kilicho mali yao, la sivyo mtafagiliwa mbali kwa sababu ya dhambi zao zote.”
27
Hivyo wakaondoka karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu walikuwa wametoka nje, nao walikuwa wamesimama pamoja na wake zao, watoto wao na wale wanyonyao kwenye mlango wa mahema yao.
28
Ndipo Musa akasema, “Hivi ndivyo mtakavyojua kuwa bwana amenituma kufanya mambo haya, na kwamba halikuwa wazo langu.
29
Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basi bwana hakunituma mimi.
30
Lakini ikiwa bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau bwana.”
31
Mara Musa alipomaliza kusema haya yote, ardhi iliyokuwa chini yao ikapasuka,
32
nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na jamaa zao, na watu wote wa Kora na mali zao zote.
33
Wakashuka chini kaburini wakiwa hai, pamoja na kila kitu walichokuwa nacho; nchi ikajifunika juu yao, nao wakaangamia wakatoweka kutoka kusanyiko.
34
Kutoka kilio chao, Waisraeli wote waliowazunguka walikimbia, wakipaza sauti, “Nchi inatumeza na sisi pia!”
35
Moto ukaja kutoka kwa bwana, ukawateketeza wale watu 250 waliokuwa wakifukiza uvumba.
36
bwana akamwambia Musa,
37
“Mwambie Eleazari mwana wa kuhani Haruni, atoe vyetezo kwenye mabaki ya moto na kutawanya makaa mbali kiasi, kwa maana vyetezo ni vitakatifu:
38
vyetezo vya watu waliofanya dhambi iliyowagharimu maisha yao. Fua vyetezo hivyo kuwa bamba ili kufunika madhabahu, kwa maana vimeletwa mbele za bwana na vimekuwa vitakatifu. Navyo viwe ishara kwa Waisraeli.”
39
Hivyo kuhani Eleazari akavikusanya vile vyetezo vya shaba vilivyoletwa na wale waliokuwa wameteketezwa kwa moto, naye akavifua kufunika madhabahu,
40
kama vile bwana alivyomwelekeza kupitia Musa. Hili lilikuwa kuwakumbusha Waisraeli kwamba hakuna mtu hata mmoja, isipokuwa mzao wa Haruni, awezaye kuja kufukiza uvumba mbele za bwana, la sivyo, angekuwa kama Kora na wafuasi wake.
41
Siku iliyofuata jumuiya yote ya Kiisraeli wakanung’unika dhidi ya Musa na Haruni, wakisema, “Mmewaua watu wa bwana.”
42
Lakini wakati kusanyiko lilipokusanyika kupingana na Musa na Haruni, nalo likageuka kuelekea Hema la Kukutania, ghafula wingu likafunika Hema, nao utukufu wa bwana ukatokea.
43
Ndipo Musa na Haruni wakaenda mbele ya Hema la Kukutania,
44
naye bwana akamwambia Musa,
45
“Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi.
46
Kisha Musa akamwambia Haruni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani yake, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwa bwana, na tauni imeanza.”
47
Hivyo Haruni akafanya kama Musa alivyosema, akakimbilia katikati ya kusanyiko. Tauni ilikuwa tayari imeanza miongoni mwa watu, lakini Haruni akafukiza uvumba na kufanya upatanisho kwa ajili yao.
48
Haruni akasimama kati ya waliokuwa hai na waliokufa, nayo tauni ikakoma.
49
Lakini walikufa watu 14,700 kutokana na tauni hiyo, licha ya wale waliokuwa wamekufa kwa sababu ya Kora.
50
Ndipo Haruni akamrudia Musa kwenye mlango wa Hema la Kukutania, kwa maana tauni ilikuwa imekoma.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36