bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Numbers 31
Numbers 31
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 32 →
1
bwana akamwambia Musa,
2
“Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.”
3
Kwa hiyo Musa akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha bwana.
4
Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.”
5
Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli.
6
Musa aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria.
7
Walipigana dhidi ya Wamidiani, kama bwana alivyomwagiza Musa, nao waliua kila mwanaume.
8
Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vilevile walimuua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga.
9
Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali zao kama nyara.
10
Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote.
11
Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama,
12
nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Musa na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.
13
Musa, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.
14
Musa aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.
15
Musa akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?”
16
“Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasi bwana kwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu wa bwana.
17
Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa,
18
lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.
19
“Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.
20
Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”
21
Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayo bwana alimpa Musa:
22
Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi,
23
na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.
24
Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”
25
bwana akamwambia Musa,
26
“Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa.
27
Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.
28
Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo au mbuzi.
29
Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya bwana.
30
Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya bwana.”
31
Kwa hiyo Musa na kuhani Eleazari wakafanya kama bwana alivyomwagiza Musa.
32
Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,
33
ng’ombe 72,000,
34
punda 61,000,
35
na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.
36
Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa: Kondoo 337,500
37
ambayo ushuru kwa ajili ya bwana ilikuwa kondoo 675;
38
ng’ombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya bwana ulikuwa ng’ombe 72;
39
punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya bwana ulikuwa punda 61;
40
Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya bwana ulikuwa watu 32.
41
Musa alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya bwana, kama bwana alivyomwagiza Musa.
42
Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Musa aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani,
43
nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500,
44
ng’ombe 36,000,
45
punda 30,500,
46
na wanadamu 16,000.
47
Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Musa alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya bwana.
48
Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Musa
49
na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana.
50
Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za bwana.”
51
Musa na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa.
52
Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Musa na kuhani Eleazari walimletea bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,750.
53
Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi.
54
Musa na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele za bwana.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 32 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36