bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Numbers 2
Numbers 2
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 3 →
1
BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
2
Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye bendera yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote.
3
Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea mawio ya jua, ndio wale wa bendera ya kambi ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.
4
Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sabini na nne na mia sita.
5
Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila la Isakari; na mkuu wa wana wa Isakari atakuwa Nethaneli mwana wa Suari;
6
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na nne na mia nne;
7
na kabila la Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni;
8
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na saba na mia nne.
9
Hao wote waliohesabiwa katika kambi ya Yuda walikuwa elfu mia moja themanini na sita na mia nne, kwa makundi yao. Hao ndio watakaotangulia mbele.
10
Upande wa kusini kutakuwa na bendera ya kambi ya Reubeni kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Reubeni atakuwa Elisuri mwana wa Shedeuri.
11
Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu arobaini na sita na mia tano.
12
Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila la Simeoni; na mkuu wa wana wa Simeoni atakuwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai;
13
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na tisa na mia tatu;
14
na kabila la Gadi; na mkuu wa wana wa Gadi atakuwa Eliasafu mwana wa Deueli;
15
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu arobaini na tano, mia sita na hamsini.
16
Wote waliohesabiwa katika kambi za Reubeni walikuwa elfu mia moja hamsini na moja na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaofuata wakiwa kundi la pili.
17
Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na kambi za Walawi katikati ya kambi zote; kama wapangavyo kambi, watasafiri vivyo hivyo, kila mtu mahali pake, penye bendera zao.
18
Upande wa magharibi kutakuwa na bendera ya kambi ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi.
19
Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arobaini na mia tano.
20
Na karibu naye itakuwa kabila la Manase; na mkuu wa wana wa Manase atakuwa Gamalieli mwana wa Pedasuri;
21
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu thelathini na mbili na mia mbili;
22
tena kabila la Benyamini; na mkuu wa wana wa Benyamini atakuwa Abidani mwana wa Gideoni;
23
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu thelathini na tano na mia nne.
24
Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu walikuwa elfu mia moja na nane na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaoondoka wakiwa kundi la tatu.
25
Upande wa kaskazini kutakuwa na bendera ya kambi ya Dani kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Dani atakuwa Ahiezeri mwana wa Amishadai.
26
Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na mbili na mia saba.
27
Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila la Asheri; na mkuu wa wana wa Asheri atakuwa Pagieli mwana wa Okrani;
28
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu arobaini na moja na mia tano;
29
kisha kabila la Naftali; na mkuu wa wana wa Naftali atakuwa Ahira mwana wa Enani;
30
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na tatu na mia nne.
31
Wote waliohesabiwa katika kambi ya Dani walikuwa elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Hao ndio watakaoondoka mwisho kwa kufuata bendera yao.
32
Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa nyumba za baba zao; wote waliohesabiwa katika kambi kwa majeshi yao, walikuwa elfu mia sita na tatu na mia tano na hamsini.
33
Lakini Walawi hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
34
Hivyo ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama BWANA alivyomwamuru Musa; ndivyo walivyojipanga kufuata bendera zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36