bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Numbers 29
Numbers 29
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 30 →
1
Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu.
2
Nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja wote wasiwe na dosari;
3
pamoja na sadaka yake ya unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi ya ng'ombe, sehemu ya mbili ya kumi kwa kondoo dume,
4
na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba;
5
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu;
6
zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto.
7
Tena siku ya kumi ya huo mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; nanyi mtajinyima nafsi zenu, msifanye kazi yoyote ya utumishi
8
lakini mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja; watakuwa wakamilifu kwenu;
9
pamoja na sadaka zake za unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi kwa huyo ng'ombe, na sehemu ya mbili ya kumi kwa huyo kondoo,
10
na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba;
11
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
12
Tena siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote kwenye nafsi zenu, nanyi mtamfanyia BWANA sikukuu muda wa siku saba;
13
nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume wachanga kumi na watatu na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu;
14
pamoja na sadaka zake za unga, unga laini uliochanganywa na mafuta, sehemu ya tatu ya kumi kwa kila ng'ombe katika wale kumi na watatu na sehemu ya mbili ya kumi kwa kila kondoo katika hao kondoo dume wawili;
15
na sehemu ya moja ya kumi kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo kumi na wanne;
16
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
17
Tena siku ya pili mtasongeza ng'ombe dume wachanga kumi na wawili, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja kumi na wanne wakamilifu;
18
pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri hiyo;
19
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
20
Tena siku ya tatu mtasongeza ng'ombe dume kumi na mmoja, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne;
21
pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo kama idadi yao ilivyo kulingana na amri;
22
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
23
Tena siku ya nne mtasongeza ng'ombe dume kumi, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne;
24
na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri;
25
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
26
Tena siku ya tano mtasongeza ng'ombe dume tisa, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne;
27
pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri;
28
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
29
Tena siku ya sita mtasongeza ng'ombe dume wanane, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne;
30
pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri;
31
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
32
Tena siku ya saba mtasongeza ng'ombe dume saba, na kondoo dume wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari kumi na wanne;
33
pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng'ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri;
34
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
35
Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yoyote kwenye nafsi zenu;
36
lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng'ombe dume mmoja, na kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja wasio na dosari saba;
37
pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa huyo ng'ombe, na kwa huyo kondoo dume, na kwa wale wana-kondoo, kama idadi yao ilivyo, kulingana na amri;
38
na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
39
Sadaka hizo mtamsogezea BWANA katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani.
40
Naye Musa akawaambia wana wa Israeli vile vile kama hayo yote BWANA alivyomwagiza Musa.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36