bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Esther 6
Esther 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 7 →
1
Usiku ule mfalme hakupata usingizi, akaagiza, wamletee hicho kitabu cha mambo ya siku yapasayo kukumbukwa. Ikawa, yaliposomwa masikioni pa mfalme,
2
zikaoneka zile habari zilizoandikwa za kwamba: Mordekai ameumbua watumishi wa nyumbani mwa mfalme, Bigitana na Teresi, waliokuwa walinda mlango, waliotafuta njia ya kumwua mfalme Ahaswerosi kwa mikono yao.
3
Mfalme akauliza: Mordekai amepata tunzo gani au ukuu gani kwa tendo hilo? Vijana wa mfalme waliomtumikia wakajibu: Hakuna alichofanyiziwa.
4
Mfalme akauliza tena: Uani yuko nani? Naye Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aje kumwambia mfalme, wamtundike Mordekai katika ule mti, aliomsimikia.
5
Vijana wa mfalme walipomwambia: Tazama, ni Hamani anayesimama uani, mfalme akasema: Aje!
6
Hamani alipokuja, mfalme akamwuliza: Mfalme akipendezwa kumheshimu mtu, atafanyiziwa nini huyo mtu? Hamani akawaza moyoni mwake kwamba: Yuko nani, mfalme apendezwaye naye, amheshimu, nisipokuwa mimi?
7
Kwa hiyo Hamani akamwambia mfalme: Kama yuko mtu, mfalme apendezwaye naye, amheshimu,
8
na walete nguo ya kifalme, mfalme aliyoivaa, na farasi, mfalme aliyempanda, aliyevikwa kichwani pake kilemba cha kifalme!
9
Kisha mkuu mmoja wa mfalme mwenye macheo apewe hiyo nguo na huyo farasi, wamvike huyo mtu, mfalme apendezwaye naye, amheshimu, kisha wampandishe huyo farasi uwanjani mwa mji na kupiga mbiu mbele yake kwamba: Hivi ndivyo, mtu anavyofanyiziwa, mfalme akipendezwa naye, amheshimu.
10
Ndipo, mfalme alipomwambia Hamani: Nenda upesi sasa hivi kuichukua hiyo nguo na huyo farasi, kama ulivyosema, umfanyizie vivyo hivyo Myuda Mordekai akaaye langoni kwa mfalme! Lakini usisahau hata neno moja katika hayo, uliyoyasema!
11
Basi, Hamani akaichukua hiyo nguo na huyo farasi, akamvika Mordekai, kisha akampandisha uwanjani mwa mji, akapiga mbiu mbele yake kwamba: Hivi ndivyo, mtu anavyofanyiziwa, mfalme akipendezwa naye, amheshimu.
12
Kisha Mordekai akarudi langoni pake kwa mfalme, lakini Hamani akaikimbilia nyumba yake kwa kusikitika, akawa amejifunika kichwa.
13
Hamani akamsimulia mkewe na wapenzi wake yote yaliyomtukia. Rafiki zake waliokuwa werevu wa kweli na mkewe Zeresi wakamwambia: Kama huyu Mordekai, uliyeanza kumwangukia, ni wa kizazi cha Wayuda, hutamshinda, ila utaendelea kumwangukia.
14
Walipokuwa wangali wakisema naye, wakafika watumishi wa nyumbani wa mfalme, wakamhimiza Hamani, aje upesi kula karamu, Esteri aliyoifanya.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10