bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Esther 7
Esther 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 8 →
1
Mfalme akaja pamoja na Hamani karamuni kwake Esteri, mkewe mfalme.
2
Walipokunywa mvinyo, mfalme akamwuliza Esteri nayo siku hiyo ya pili: Unaomba nini, Esteri, mkewe mfalme? Utapewa. Unataka nini? Ingawa ni nusu ya ufalme, itafanyika.
3
Ndipo, Esteri, mkewe mfalme, alipomjibu akisema: Kama nimeona upendeleo mbele yako, mfalme, navyo vikiwa vema kwako, mfalme, nipewe roho yangu kwa kuomba kwangu! Tena nipewe wenzangu wa ukoo kwa kutaka kwangu!
4
Kwani tumekwisha kuuzwa mimi na wenzangu wa ukoo, tutoweshwe kwa kuuawa na kwa kuangamizwa. Kama tungaliuzwa tu kuwa watumwa na vijakazi, ningalinyamaza; lakini mpingani huyo hawezi kuvilipa, mfalme akipotelewa na watu hao.
5
Mfalme Ahaswerosi akamwuliza Esteri, mkewe mfalme, na kusema: Ni nani huyu, tena yuko wapi aliyeushupaza moyo wake, upate kuwaza tendo kama hilo?
6
Esteri akamwambia: Mtu wetu mpingani na adui ni huyu Hamani, ni mbaya. Ndipo, Hamani alipostuka mbele ya mfalme na mkewe mfalme.
7
Lakini mfalme akainuka kwa makali hapo penye mvinyo, akaja bustanini kwenye jumba lake. Naye Hamani akasimama kumwomba Esteri, mkewe mfalme, amponye, kwani ameona, ya kuwa liko shauri baya, alilokwisha kukatiwa na mfalme.
8
Mfalme alipotoka kule bustanini kwenye jumba lake na kuingia tena mle nyumbani, waliomkunywa mvinyo, Hamani alikuwa ameanguka penye kitanda, Esteri alipokaa; ndipo, mfalme aliposema: Je, Naye mkewe mfalme anataka kumkorofisha humu nyumbani mwangu? Neno hili lilipotoka kinywani mwa mfalme, ndipo, walipoufunika uso wa Hamani.
9
Harbona, mmoja wao watumishi wa nyumbani waliomtumikia mfalme, akasema: Tazameni, ule mti, Hamani aliomsimikia Mordekai aliyesema mema ya kumponya mfalme, ungaliko kwenye nyumba ya Hamani, ni ule mrefu wa mikono hamsini. Ndipo, mfalme aliposema: Haya! Mtundikeni mumo humo!
10
Wakamtundika Hamani katika ule mti, aliomsimikia Mordekai; kisha makali ya mfalme yakatulia.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10