bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joel 2
Joel 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
1
Pigeni baragumu Sioni! Pigeni kelele milimani kwenye utakatifu wangu! Wote wakaao katika nchi hii watetemeke, kwa kuwa siku ya Bwana inakuja, iko karibu!
2
Ni siku yenye giza lililozidi kabisa, ni siku yenye mawingu yaliyo meusi; kama wekundu wa kupambazuka unavyotandama milimani juu, ndivyo, lile kabila linavyotokeza wengi walio wenye nguvu; walio kama hao hawakuwako toka kale, wala hawatakuwako tena nyuma yao hata miaka ya vizazi na vizazi.
3
Mbele yao moto unakula, nyuma yao miali ya moto inawaka; mbele yao nchi ni kama bustani ya Edeni, nyuma yao ni jangwa tupu, pasipatikane pa kuponea.
4
Ukiwatazama, wanafanana kuwa kama farasi, wanapiga mbio kama wapanda farasi.
5
Uvumi wao ni kama wa magari yarukayo milimani juu au kama uvumi wa moto ulao majani makavu; ni kama wa watu wenye nguvu waliojipanga kupigana.
6
Mbele yao watu wanajipinda, nyuso zao zikiwapoa.
7
Wanapiga mbio kama wenye nguvu wa vitani, wanakwea ukutani kama mafundi wa mapigano, wanakwenda kila mmoja katika njia yake, hawayapotoi kamwe mapito yao,
8
wala hawasukumani wenyewe mtu na ndugu yake, kila mmoja huendelea katika mkondo wake; ingawa wengine wao waanguke kwa kupigwa, hawazuiliki.
9
Wanaurukia mji wakizikwea kuta za bomani mbiombio, wanapanda kuingia nyumbani na kujipenyeza madirishani kama mwizi.
10
Mbele yao nchi inatetemeka, nazo mbingu zinatikisika, jua na mwezi unaguiwa na giza, nazo nyota zinakoma kuangaza.
11
Bwana anapiga ngurumo yake, ivitangulie vikosi vyake, kwa kuwa kambi lake ni kubwa sana, nao walitimizao neno lake ni wenye nguvu; kwani siku ya Bwana ni kuu, inaogopesha sana, yuko nani atakayeivumilia?
12
Ndivyo, asemavyo Bwana: Sasa hivi rudini kwangu kwa mioyo yenu yote mkifunga kwa kulia na kuomboleza!
13
Irarueni mioyo yenu, msiyararue mavazi yenu! Kisha rudini kwa Bwana Mungu wenu! Kwani Yeye ni mwenye utu na huruma, tena mwenye uvumilivu na upole mwingi; hugeuza moyo, asifanye mabaya.
14
Labda atageuza moyo tena, atuachilie mbaraka atakapoondoka, akiwapatia vilaji na vinywaji vya kumtambikia Bwana mungu wenu!
15
Pigeni baragumu Sioni! Eueni mfungo! Utangazeni mkutano!
16
Wakusanyeni watu wa kwenu! Ueueni huo mkutano! Waiteni wazee! Wakusanyeni nao wachanga, nao wanyonyao maziwa! Mchumba mume atoke chumbani mwake! Naye mchumba mke atoke mwake, alimo!
17
Watambikaji wanaomtumikia Bwana na walie katikati ya ukumbi na meza ya kutambikia, waseme: Bwana, wahurumie walio ukoo wako! Usiwatoe walio fungu lako, watukanwe, wamizimu wakiwatawala! Mbona wataka, waseme kwa makabila mengine: Mungu wao yuko wapi?
18
Ndipo, Bwana alipoionea nchi yake wivu, akawahurumia walio ukoo wake.
19
Bwana akajibu na kuwaambia walio ukoo wake: Mtaniona, nikiwapatia ngano na pombe mbichi na mafuta, myashibe! Sitawatoa tena, mtukanwe na wamizimu.
20
Nao wale waliotoka kaskazini nitawaondoa kwenu, niwapeleke mbali, niwakumbe, waende katika nchi kavu iliyo peke yake; watangulizi wao nitawatupa katika bahari iliyoko upande wa maawioni kwa jua, wafuasi wao wa nyuma nitawatupa katika bahari iliyoko upande wa machweoni kwa jua, mnuko mbaya wa kuoza kwao utapanda juu, kwa sababu watakuwa wamefanya makuu zaidi.
21
Usiogope, wewe nchi! Ila shangilia kwa furaha! Kwani Bwana atafanya jambo kuu.
22
Msiogope, ninyi nyama wa porini! Kwani mbuga za nyikani zitachipuka, kwani miti itazaa matunda yao, nayo mikuyu na mizabibu itatoa mazao ya nguvu.
23
Wana wa Sioni, shangilieni! Mfurahieni Bwana Mungu wenu! Kwani anawapa mvua ya masika hapo ipasapo, anawanyeshea kwanza mvua za masika nazo za vuli.
24
Ndipo, penye kupuria patakapojaa ngano, nayo makamulio yatafurikiwa na mvinyo mbichi na mafuta.
25
Nitawarudishia miaka iliyoliwa nao nzige na funutu na bumundu na panzi, ni vile vikosi vyangu vingi vyenye nguvu, nilivyovituma kwenu.
26
Mtakula kabisa na kushiba, mlisifu Jina la Bwana Mungu wenu, kwa kuwa alifanya kwenu mataajabu! Kweli walio ukoo wangu hawatapatwa na soni kale na kale.
27
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi niko katikati ya Waisiraeli, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wenu, siye mwingine. Kweli walio ukoo wangu hawatapatwa na soni kale na kale.
28
Hayo yatakapokwisha, ndipo, itakapokuwa, niwamiminie Roho yangu wote walio wenye miili ya kimtu. Nao wana wenu wa kiume na wa kike watasema na kufumbua; nao wazee wenu wataoteshwa ndoto, nao vijana wenu wataona maono.
29
Nao walio watumwa wangu waume na wake nitawamiminia Roho yangu siku zilezile.
30
Nami nitafanya vioja mbinguni na nchini, vyenye damu na moto na moshimoshi.
31
Jua litageuka, liwe giza, nao mwezi utageuka, uwe damu mbele ya kutimia kwake ile siku kubwa ya Bwana, inayoogopesha.
32
Tena itakuwa, kila atakayelitambikia Jina la Bwana ataokoka. Kwani mlimani pa Sioni namo Yerusalemu watakuwamo waliopona, kama Bwana alivyosema; namo miongoni mwao waliookolewa watakuwamo, Bwana aliowaita.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3