bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joel 3
Joel 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
1
Siku zile za huo wakati zitakapotimia, mtaniona nikiyafungua mafungo ya Yuda na ya Yerusalemu.
2
Ndipo, nitakapowakusanya wamizimu wote, niwapeleke katika bonde la Yosafati; ndiko, nitakakowakatia shauri kwa ajili ya ukoo wangu wa Isiraeli ulio fungu langu, kwa kuwa wamewatawanya kwenye wamizimu, wakajigawanyia nchi yangu.
3
Wao walio ukoo wangu wamewapigia kura, wakitoa mtoto wa kiume, wajipatie mwanamke mgoni, tena wamenunua mvinyo kwa mtoto wa kike, wakazinywa.
4
Ninyi wa Tiro na wa Sidoni mwanitakiaje? Nanyi nyote mkaao upande wa Wafilisti? Je? Ninyi mwataka kunilipisha niliyofanyiziwa? Au mnacho, mtakacho kunifanyizia? Sasa hivi kwa upesi nitawarudishia matendo yenu, yaje kuwaangukia vichwani penu.
5
Kwani mmezichukua fedha zangu na dhahabu zangu, nayo mapambo mazuri yaliyonipendeza mmeyapeleka katika majumba ya miungu yenu.
6
Nao wana wa Yuda na wa Yerusalemu mmewauzia wana wa Wagriki, mpate kuwapeleka mbali, wasirudi mipakani kwao.
7
Lakini mtaniona, nikiwainua mahali hapo, mlipowauzia, nitakapowarudishia matendo yenu, yaje kuwaangukia vichwani penu.
8
Kisha nitawauza wana wenu wa kiume na wa kike na kuwatia mikononi mwao wana wa Yuda, nao watawauzia Wasaba, kwa kuwa ni taifa likaalo mbali; kwani Bwana ndiye aliyevisema.
9
Yatangazeni haya kwa mataifa! Kisha eueni vita! Wainueni wenye nguvu! Wote walio mafundi wa vita na waje na kujipanga!
10
Yafueni majembe yenu, yawe panga, navyo visu vyenu, viwe mikuki! Naye aliye mnyonge sharti aseme: Mimi ni mwenye nguvu!
11
Pigeni mbio, mje mkusanyike, ninyi mataifa yote mkaao na kuwazunguka! Nawe Bwana, wapeleke wanguvu wako, wawatelemkie kuko huko!
12
Mataifa na waimbe, waje huko bondeni kwa Yosafati! Kwani ndiko, nitakakokaa, niwahukumu wao wa mataifa yote wakaao na kuwazunguka.
13
Haya! Leteni miundu! Kwani mavuno yameiva. Njoni, mkanyage! Kwani kamulio limejaa, mapipa nayo yanamwagikia, kwani mabaya yao ni mengi.
14
Yako makundi ya watu mengi na mengi huko bondeni kunakokatwa mashauri, kwani siku ya Bwana iko karibu huko bondeni kunakokatwa mashauri.
15
Jua na mwezi umeguiwa na giza, nazo nyota zimekoma kuangaza.
16
Ndipo, Bwana atakaponguruma mle Sioni, ataivumisha sauti yake mle Yerusalemu, mbingu na nchi zitetemeke. Lakini Bwana atakuwa kimbilio lao walio ukoo wake na ngome yao walio wana wa Isiraeli.
17
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wenu akaaye Sioni penye mlima wangu mtakatifu. Nao Yerusalemu utakuwa mji mtakatifu, msimopita wageni tena.
18
Siku ile itakuwa, milima idondoe mvinyo mbichi, navyo vilima vitachuruzika maziwa, navyo vijito vyote vya Yuda vitaleta maji mengi. Kisha Nyumbani mwa Bwana mtatokea chemchemi, italinywesha Bonde la Migunda.
19
Misri itakuwa mapori tu, nayo Edomu itakuwa nyika yenye mapori matupu, kwa kuwa wamewakorofisha wana wa Yuda, wakamwaga katika nchi yao damu zao wasiokosa.
20
Lakini Yuda itakaa watu kale na kale, namo Yerusalemu watakaa vizazi kwa vizazi.
21
Ndivyo, nitakavyozilipiza damu zao, ambazo sikuzilipiza bado. Naye Bwana atakuwa anakaa Sioni!
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
All chapters:
1
2
3