bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Titus 2
Titus 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
1
Lakini wewe sema yapatanayo na ufundisho utupao uzima!
2
Waume wazee sharti wawe watu wasiokunywa kileo, wapewe macheo, wawe werevu wa kweli, wajipatie uzima kwa kumtegemea Mungu na kwa kupendana na kwa kuvumilia kwao!
3
Vivyo hivyo wanawake wazee nao sharti wafanye mwenendo uwapasao walio watakatifu! Wasisengenye wala wasiwe watumwa wa unywaji wa pombe nyingi, ila wenye kufundisha wengine yaliyo mazuri,
4
wapate kuwaerevusha wanawake walio vijana bado, wawapende waume na watoto wao!
5
Hivyo nao wake vijana watakuwa werevu wa kweli, wang'avu, wenye kutengeneza nyumba zao vizuri, wenye wema na wenye kuwatii waume wao, Neno la Mungu lisibezwe.
6
Lakini vilevile waambie vijana waume na kuwakanya, waerevuke kweli!
7
Katika mambo yote ujiweke mwenyewe kuwawia kielezo cha kujifundishia matendo mazuri! Wafundishe kujiangalia miili, waipe macheo yaipasayo!
8
Litangaze Neno litupalo uzima lisilobishika, mpingani aingiwe na soni, asiweze kusema neno ovu lo lote la kutusuta!
9
Walio watumwa waambie, wawatii mabwana zao, wawapendeze katika mambo yote, wasiwe wabishi,
10
wasiibe ila wajionyeshe kuwa wenye welekevu na wema wote, matendo yao yote yawe mapambo ya ufundisho wa mwokozi na Mungu wetu!
11
*Kwani mema yake Mungu, ayagawiayo watu wote ya kuwaokoa, yametokea waziwazi,
12
nayo hutuonya, tuuvunje mwenendo wa kimizimu, tusizifuate tamaa za humu ulimwenguni, ila siku hizi za sasa za kuishi duniani tuwe wenye werevu wa kweli na wenye wongofu na wenye kumcha Mungu.
13
Kisha tuchungue, kingojeo chetu cha kutushangiliza kitakavyotimia, utukufu wa Mungu wetu mkuu na wa mwokozi wetu Kristo Yesu utakapotokea.
14
Yeye ndiye aliyejitoa mwenyewe kwa ajili yetu kuwa kole ya kuyalipa mapotovu yote, ajipatie watu wang'avu watakaokuwa wake wenye bidii ya kufanya kazi nzuri.*
15
Hayo yaseme na kuwaonya na kuwashinda wakosaji kwa nguvu zote! Mtu asikubeze
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3