bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Titus 3
Titus 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
1
Wakumbushe wajinyenyekeze penye wakuu na wenye nguvu, wamtii na kujiweka tayari kufanya kazi njema zo zote!
2
Wasitukane mtu, wala wasichokoze wenyewe, ila wajionyeshe kuwa wenye mambo yapasayo, wawaendee watu wote kwa upole kabisa!
3
Kwani hata sisi kale tulikuwa wapumbavu waliokataa kutii; tulikuwa tumepotea, tukazitumikia tamaa nyingi zilizotupendeza, tukaendelea kuwa wenye maovu na wivu na machukivu ya kuchukiana sisi kwa sisi.
4
*Ndipo, ulipotutokea utu wake mwokozi na Mungu wetu aliyetupenda sisi watu,
5
akatuokoa sisi, lakini si kwa sababu ya matendo ya wongofu, tuliyofanya sisi; ila kwa huruma yake yeye alituponya akituosha maji ya kutuzaa mara ya pili, tukawa watu wapya kwa kupewa Roho takatifu;
6
hii ndiyo aliyotumiminia, ikatifurikia, alipomtuma mwokozi wetu Yesu Kristo.
7
Kwa mema yake yeye, aliyotugawia, tukapata wongofu, tukawekewa nasi urithi wetu penye uzima wa kale na kale, kama tunavyongojea.*
8
Hili neno ni la kweli. Nami nataka, mambo haya uyafundishe kwa nguvu ya kuwashinda, maana wale waliomtegemea Mungu wazitunze kazi zao, ziwe nzuri kuliko za wengine. Haya ni mazuri, nayo huwafalia watu.
9
Lakini mabishano ya upuzi na mambo ya wakale na machokozi na magomvi ya miiko uyaache! Kwani hayafai kitu, ni ya bure tu.
10
Mtu mzushi mwonye mara moja, hata mara mbili! Asipoonyeka, mwepuke!
11
Ujue: Mtu aliye hivyo amekwisha kutengeka, tena hujipatia hukumu mwenyewe kwa kukosa kwake.
12
Nitakapomtuma kwako Artema au Tikiko, jikaze kuja kwangu huku Nikopoli! Kwani ndiko, ninakotaka kuzimaliza siku hizi za kipupwe.
13
Akina Zena aliye mjuzi wa Maonyo na Apolo watume upesi, waende zao; lakini uwatunzie vema, wasikose yawapasayo njiani!
14
Hapo wa kwetu nao wajifunze kufanya kazi zilizo nzuri kuliko za wengine! Ikiwa wanatakwa, na wapatie wengine yatakayowatunza, wasifanane na miti isiyozaa!
15
Wanakusalimu wote walio pamoja nami. Wasalimu wanaotupenda kwa kuwa wenye kumtegemea Mungu! Upole uwakalie ninyi nyote! Amin.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
All chapters:
1
2
3