bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Isaiah 33
Isaiah 33
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 34 →
1
Ole kwako! Unaangamiza ingawa hauangamizwi. Unadanganya ingawa haudanganywi. Utakapokwisha kuangamiza, wewe utaangamizwa! Utakapomaliza kudanganya, wewe utadanganywa.
2
Ee Yawe, utuonee huruma, kwako tumeliweka tumaini letu. Ukuwe kikingio chetu kila siku, mwokozi wetu wakati wa taabu.
3
Kwa kishindo cha sauti yako watu wanakimbia; unaposimama tu, mataifa yanatawanyika.
4
Waadui zao wanakusanya vitu walivyonyanganya, wanavirukia kama mapanzi.
5
Yawe ametukuzwa, yeye anaishi juu mbinguni. Ameujaza Sayuni usawa na haki.
6
Enyi watu wa Yerusalema, Yawe atawajalia usalama, atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa. Akiba yenu kubwa ni kumwogopa Yawe.
7
Muangalie, washujaa wao wanalia, wajumbe wa amani wanaomboleza.
8
Barabara kubwa zimebaki tupu; hakuna anayesafiri kupitia ndani yao. Mapatano yanavunjwa ovyo, washuhuda wanazarauliwa. Hakuna anayejali tena maisha ya wanadamu.
9
Inchi inaomboleza na kunyauka; pori ya Lebanoni imekauka, bonde zuri la Saroni limekuwa jangwa, kule Basani na mulima Karmeli majani yote yamekauka.
10
Yawe anasema hivi: Sasa mimi nitasimama; sasa nitajiweka tayari; sasa mimi nitatukuzwa.
11
Mipango yenu yote ni kama maganda, na matokeo yake ni takataka tupu. Pumzi yangu itawaangamiza kama moto.
12
Watu watakuwa kama wamechomwa kuwa majivu, kama miiba iliyokatwa na kuteketezwa katika moto.
13
Musikilize mambo muliyofanya, enyi munaokuwa mbali; nanyi munaokuwa karibu, mutambue uwezo wangu.
14
Wenye zambi katika Sayuni wanaogopa, wasiomwamini Mungu wanatetemeka na kusema: Nani anayeweza kuvumilia moto huu mukali? Nani anayeweza kuvumilia ndimi za moto usiozimika?
15
Ni mutu anayekuwa hivi: anaishi kwa haki na kusema kwa usawa, anazarau kabisa utajiri wa unyanganyi, anakataa kupokea kituliro, hakubali hata kidogo kusikia mipango ya mauaji, wala hakubali macho yake yaone maovu.
16
Mutu wa namna hiyo anaishi kwenye nafasi ya juu, pahali salama, penye pango na mawe makubwa; atapewa chakula chake siku zote, na maji yake ya kunywa hayatakosekana.
17
Mutaweza kumwona mufalme katika utukufu wake, mutaiona inchi anayotawala, kubwa na pana.
18
Mutakumbuka kitisho kilichopita na kujiuliza: Wako wapi wale waliokadirisha na kuchunguza kodi? Wako wapi wale waliopeleleza ugumu wa kuta zetu?
19
Hamutawaona tena watu wale wenye kiburi, wanaozungumuza luga isiyoeleweka.
20
Muangalie Sayuni tunamofanyia sikukuu zetu; muangalie Yerusalema, makao matulivu, hema imara; misumari yake haitaongolewa hata kidogo, kamba zake hazitakatwa hata moja.
21
Humo Yawe atatuonyesha ukubwa wake. Kutakuwa mito mikubwa na vijito, lakini mashua za vita hazitapita, wala mashua kubwa kuingia.
22
Maana Yawe ni mwamuzi wetu, yeye ni mutawala wetu; Yawe ni mufalme wetu, yeye ndiye anayetuokoa.
23
Ewe Sayuni, kamba zako zimeregea, haziwezi kushikilia matanga yake, wala kufungia paa zao. Lakini vitu vingi vilivyonyanganywa vitagawanywa; hata vilema wataweza kupata sehemu yao.
24
Hakuna atakayesema tena ni mugonjwa; watu watasamehewa uovu wao wote.
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66