bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Hosea 10
Hosea 10
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 11 →
1
Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri, mzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu. Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.
2
Mioyo yao imejaa udanganyifu. Sasa ni lazima wawajibike kwa hatia yao. Mwenyezi-Mungu atazibomoa madhabahu zao na kuziharibu nguzo zao.
3
Wakati huo watasema: “Hatuna tena mfalme, kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu; lakini, naye mfalme atatufanyia nini?”
4
Wanachosema ni maneno matupu; wanaapa na kufanya mikataba ya bure; haki imekuwa si haki tena, inachipua kama magugu ya sumu shambani.
5
Wakazi wa Samaria watatetemeka kwa sababu ya ndama wa huko Betheli. Watu wake watamwombolezea ndama huyo, hata makuhani wanaomwabudu watamlilia; kwani fahari ya ndama huyo imeondolewa.
6
Kinyago hicho kitapelekwa Ashuru, kama ushuru kwa mfalme mkuu. Watu wa Efraimu wataaibishwa, Waisraeli watakionea aibu kinyago chao.
7
Mfalme wa Samaria atachukuliwa, kama kipande cha mti juu ya maji.
8
Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni, dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa. Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao. Nao wataiambia milima, “Tufunikeni” na vilima, “Tuangukieni!”
9
Enyi Waisraeli, nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea, na bado mnaendelea. Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.
10
Nitawajia watu hawa wapotovu na kuwaadhibu; watu wa mataifa watakusanyika kuwashambulia, watakapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao nyingi.
11
Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri, akapenda kupura nafaka. Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira. Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe, naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.
12
Pandeni wema kwa faida yenu, nanyi mtavuna upendo; limeni mashamba yaliyoachwa, maana wakati wa kunitafuta mimi Bwana umefika nami nitawanyeshea baraka.
13
Lakini nyinyi mmepanda uovu, nyinyi mmevuna dhuluma; mmekula matunda ya uongo wenu. Wewe Israeli ulitegemea nguvu zako mwenyewe, na wingi wa askari wako.
14
Kwa hiyo msukosuko wa vita utawajia watu wako; ngome zako zote zitaharibiwa, kama Shalmani alivyoharibu Beth-arbeli vitani, kina mama wakapondwa pamoja na watoto wao.
15
Ndivyo itakavyokuwa kwenu enyi watu wa Betheli, kwa sababu ya uovu wenu mkuu. Kutakapopambazuka mfalme wa Israeli atawatokomeza.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14