bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Hosea 7
Hosea 7
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
1
Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu, ninapotaka kuwaponya Waisraeli, uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa, matendo mabaya ya Samaria hujitokeza. Wao huongozwa na udanganyifu, kwenye nyumba wezi huvunja nje barabarani wanyang'anyi huvamia.
2
Hawafikiri hata kidogo kwamba mimi nayakumbuka maovu yao yote. Sasa maovu yao yamewabana. Yote waliyotenda yako mbele yangu.
3
“Wanamfurahisha mfalme kwa maovu yao wanawafurahisha wakuu kwa uhaini wao.
4
Wote ni wazinzi; wao ni kama tanuri iliyowashwa moto ambao mwokaji hauchochei tangu akande unga mpaka mkate utakapoumuka.
5
Kwenye sikukuu ya mfalme, waliwalewesha sana maofisa wake; naye mfalme akashirikiana na wahuni.
6
Kama tanuri iwakavyo, mioyo yao huwaka kwa hila; usiku kucha hasira yao hufuka moshi, ifikapo asubuhi, hulipuka kama miali ya moto.
7
Wote wamewaka hasira kama tanuri, na wanawaangamiza watawala wao. Wafalme wao wote wameanguka, wala hakuna anayeniomba msaada.
8
“Efraimu amechanganyika na watu wa mataifa. Anaonekana kama mkate ambao haukugeuzwa.
9
Wageni wamezinyonya nguvu zake, wala yeye mwenyewe hajui; mvi zimetapakaa kichwani mwake, lakini mwenyewe hana habari.
10
Kiburi cha Waisraeli chashuhudia dhidi yao, hawanirudii mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao; wala hawanitafuti kwa matukio hayo yote.
11
Efraimu ni kama njiwa, mjinga asiye na akili; mara yuko Misri, mara Ashuru kuomba.
12
Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege wa angani; nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.
13
Ole wao kwa kuwa wameniacha! Maangamizi na yawapate, maana wameniasi. Nilitaka kuwakomboa, lakini wanazua uongo dhidi yangu.
14
“Wananililia, lakini si kwa moyo. Wanagaagaa na kujikatakata vitandani mwao, kusudi nisikilize dua zao za nafaka na divai; lakini wanabaki waasi dhidi yangu.
15
Mimi ndimi niliyeiimarisha mikono yao, lakini wanafikiria maovu dhidi yangu.
16
Wanaigeukia miungu batili, wako kama uta uliolegea. Viongozi wao watakufa kwa upanga, kwa sababu ya maneno yao ya kiburi. Kwa hiyo, watadharauliwa nchini Misri.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14