bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Hosea 6
Hosea 6
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 7 →
1
“ ‘Twendeni, tukamrudie Mwenyezi-Mungu! Yeye mwenyewe ameturarua, lakini yeye mwenyewe atatuponya. Yeye mwenyewe ametujeruhi, lakini yeye mwenyewe atatibu majeraha yetu.
2
Baada ya siku mbili, atatupa uhai tena, naam, siku ya tatu atatufufua ili tuweze kuishi pamoja naye.
3
Basi tumtambue, tujitahidi kumjua Mwenyezi-Mungu. Kuja kwake ni hakika kama alfajiri, yeye atatujia kama manyunyu, kama mvua za masika ziinyweshayo ardhi.’”
4
Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitakutendea nini ee Efraimu? Nikufanyie nini ee Yuda? Upendo wenu kwangu ni kama ukungu wa asubuhi, kama umande unaotoweka upesi.
5
Ndiyo maana nimewavamia kwa njia ya manabii, nimewaangamiza kwa maneno yangu, hukumu yangu huchomoza kama pambazuko.
6
Maana ninachotaka kwenu ni upendo na si tambiko, Kumjua Mungu na si kutoa sadaka za kuteketezwa.
7
“Lakini mlilivunja agano langu kama mlivyofanya mjini Adamu; huko walinikosea uaminifu.
8
Gileadi ni mji wa waovu, umetapakaa damu.
9
Kama wanyang'anyi wamwoteavyo mtu njiani, ndivyo na makuhani walivyojikusanya na kuvizia. Wanaua watu njiani kuelekea Shekemu, naam, wanatenda uovu kupindukia.
10
Nimeona jambo la kuchukiza sana miongoni mwa Waisraeli: Watu wa Efraimu wanakimbilia miungu mingine naam, Waisraeli wamejitia unajisi.
11
Nawe Yuda hali kadhalika, nimekupangia wakati utakapovuna adhabu.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14