bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Jeremiah 16
Jeremiah 16
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 17 →
1
Kisha neno la Mwenyezi Mungu likanijia:
2
“Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.”
3
Kwa maana hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu wana wa kiume na wa kike wanaozaliwa katika nchi hii, na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao, na wale wanaume ambao ni baba zao:
4
“Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa, lakini watakuwa kama kinyesi juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa. Mizoga yao itakuwa chakula cha ndege na wanyama wa porini.”
5
Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga; usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeondoa amani yangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema Mwenyezi Mungu.
6
“Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, na hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao.
7
Hakuna yeyote atakayewapa chakula ili kuwafariji wanaoomboleza kwa ajili ya waliokufa, hata akiwa amefiwa na baba au mama, wala hakuna yeyote atakayewapa kinywaji ili kuwafariji.
8
“Usiingie katika nyumba ambayo kuna karamu, na kuketi humo ili kula na kunywa.
9
Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, aliye Mungu wa Israeli: ‘Mbele ya macho yako na katika siku zako, nitakomesha sauti zote za shangwe na za furaha, na pia sauti za bibi arusi na bwana arusi mahali hapa.’
10
“Utakapowaambia watu hawa mambo haya yote na wakakuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu ameamuru maafa makubwa kama haya dhidi yetu? Tumefanya kosa gani? Tumetenda dhambi gani dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu?’
11
Basi waambie, ‘Ni kwa sababu baba zenu waliniacha mimi, wakafuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Waliniacha mimi na hawakuishika sheria yangu,’ asema Mwenyezi Mungu.
12
‘Lakini ninyi mmetenda uovu kupita baba zenu. Tazama jinsi kila mmoja wenu anafuata ukaidi wa moyo wake mbaya, badala ya kunitii mimi.
13
Kwa hiyo nitawaondoa katika nchi hii na kuwatupa katika nchi ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua, na huko mtaitumikia miungu mingine usiku na mchana, kwa maana sitawapa fadhili zangu.’
14
“Hata hivyo, siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, “wakati watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’
15
bali watasema, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewatoa Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
16
“Lakini sasa nitawaagiza wavuvi wengi,” asema Mwenyezi Mungu, “nao watawavua. Baada ya hilo, nitawaagizia wawindaji wengi, nao watawawinda kwenye kila mlima na kilima, na katika nyufa za miamba.
17
Macho yangu yanaziona njia zao zote, hazikufichika kwangu, wala dhambi yao haikusitirika.
18
Nitawalipiza maradufu kwa ajili ya uovu wao na dhambi yao, kwa sababu wameinajisi nchi yangu kwa maumbo yasiyo na uhai ya vinyago vyao vibaya, na kuujaza urithi wangu na sanamu za kuchukiza.”
19
Ee Mwenyezi Mungu, nguvu zangu na ngome yangu, kimbilio langu wakati wa taabu, kwako mataifa watakujia kutoka miisho ya dunia na kusema, “Baba zetu hawakuwa na chochote isipokuwa miungu ya uongo, sanamu batili ambazo hazikuwafaidi kitu.
20
Je, watu hujitengenezea miungu yao wenyewe? Lakini hiyo si Mungu!”
21
“Kwa hiyo nitawafundisha: wakati huu nitawafundisha nguvu zangu na uwezo wangu. Ndipo watajua kuwa Jina langu ndimi Mwenyezi Mungu.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52