bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Jeremiah 8
Jeremiah 8
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 9 →
1
“ ‘Wakati huo, asema Mwenyezi Mungu, mifupa ya wafalme na maafisa wa Yuda, mifupa ya makuhani na manabii, na mifupa ya watu wa Yerusalemu itaondolewa kutoka makaburi yao.
2
Itawekwa wazi kwa jua, na mwezi, na nyota zote za mbingu, ambazo walizipenda na kuzitumikia, na ambazo wamezifuata kutafuta ushauri na kuziabudu. Hawatakusanywa pamoja au kuzikwa, lakini watakuwa kama kinyesi juu ya ardhi.
3
Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.’
4
“Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: “ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki? Je, mtu anapopotea harudi?
5
Kwa nini basi watu hawa waliasi? Kwa nini Yerusalemu wanaasi kila mara? Wanang’ang’ania udanganyifu na wanakataa kurudi.
6
Nimewasikiliza kwa makini, lakini hawataki kusema lililo sawa. Hakuna anayetubu makosa yake akisema, “Nimefanya nini?” Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe kama farasi anayeenda vitani.
7
Hata korongo aliye angani anayajua majira yake yaliyoamriwa, nao njiwa, mbayuwayu na koikoi hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawajui Mwenyezi Mungu anachotaka kwao.
8
“ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara kwa sababu tunayo Torati ya Mwenyezi Mungu,” wakati kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi imeandika kwa udanganyifu?
9
Wenye hekima wataaibika, watafadhaika na kunaswa. Kwa kuwa wamelikataa neno la Mwenyezi Mungu, hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?
10
Kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao, na mashamba yao kwa wamiliki wengine. Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa, wote wana tamaa ya kupata zaidi; manabii na makuhani wanafanana, wote wanafanya udanganyifu.
11
Wanafunga majeraha ya watu wangu bila uangalifu. Wanasema, “Amani, amani,” wakati hakuna amani.
12
Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? Hapana, hawana haya hata kidogo, hawajui hata kuona aibu. Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, watashushwa chini watakapoadhibiwa, asema Mwenyezi Mungu.
13
“ ‘Nitayaondoa mavuno yao, asema Mwenyezi Mungu. Hapatakuwa zabibu kwenye mzabibu. Hapatakuwa na tini kwenye mtini, na majani yake yatanyauka. Kile nilichowapa watanyang’anywa.’ ”
14
Kwa nini tunaketi hapa? Kusanyikeni pamoja! Tukimbilie kwenye miji yenye ngome, tukaangamie huko! Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ametuhukumu kuangamia, na kutupatia maji yenye sumu tunywe, kwa sababu tumemtenda dhambi.
15
Tulitegemea amani, lakini hakuna jema lililokuja, tulitegemea wakati wa kupona, lakini kulikuwa hofu tu.
16
Mkoromo wa farasi wa adui umesikika kuanzia Dani, kwa mlio wa madume yao ya farasi, nchi yote inatetemeka. Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo, mji na wote wanaoishi ndani yake.
17
“Tazama, nitatuma nyoka wenye sumu kali kati yenu, fira ambao hawawezi kulogwa, nao watawauma,” asema Mwenyezi Mungu.
18
Ee Mfariji wangu katika huzuni, moyo wangu umezimia ndani yangu.
19
Sikia kilio cha watu wangu kutoka nchi ya mbali: “Je, Mwenyezi Mungu hayuko Sayuni? Je, Mfalme wake hayuko tena huko?” “Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao, kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”
20
“Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, nasi hatujaokolewa.”
21
Kwa kuwa watu wangu wamepondwa, nami nimepondeka pia; ninaomboleza, nayo hofu kuu imenishika.
22
Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi? Je, hakuna tabibu huko? Kwa nini basi hakuna uponyaji wa majeraha ya watu wangu?
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52