bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Jeremiah 28
Jeremiah 28
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 29 →
1
Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu mbele ya makuhani na watu wote:
2
“Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.
3
Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi Mungu ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.
4
Pia nitamrudisha mahali hapa Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na wote waliohamishwa kutoka Yuda ambao walienda Babeli,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘kwa kuwa nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.’ ”
5
Ndipo nabii Yeremia akamjibu nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu.
6
Akasema, “Amen! Mwenyezi Mungu na afanye hivyo! Mwenyezi Mungu na ayatimize maneno ya unabii uliyoyatoa kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya Mwenyezi Mungu na watu wote walio uhamishoni.
7
Hata hivyo, nisikilize nikuambie yale nitakayoyasema masikioni mwako na masikioni mwa watu hawa wote:
8
Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.
9
Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa na Mwenyezi Mungu ikiwa unabii wake utatimia.”
10
Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja,
11
naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake.
12
Kitambo kidogo baada ya nabii Hanania kuivunja nira kutoka shingo ya nabii Yeremia, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia:
13
“Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma.
14
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Pia nitampa kutawala hata wanyama pori.’ ”
15
Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania! Mwenyezi Mungu hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo.
16
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Hivi karibuni nitakuondoa duniani. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Mwenyezi Mungu.’ ”
17
Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52