bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Isaiah 11
Isaiah 11
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 12 →
1
Chipukizi litatokea kutoka katika shina la Yese, kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.
2
Roho wa BWANA atakaa juu yake, Roho wa hekima na wa ufahamu, Roho wa shauri na uweza, Roho wa maarifa na wa kumcha BWANA
3
naye atafurahia kumcha BWANA. Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake, wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,
4
bali kwa adili atahukumu wahitaji, kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia. Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.
5
Haki itakuwa mkanda wake na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.
6
Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, chui atalala pamoja na mbuzi, ndama, mwana simba na ng'ombe aliyenona wa mwaka mmoja watalisha pamoja, naye mtoto mdogo atawaongoza.
7
Ng'ombe na dubu watalisha pamoja, watoto wao watalala pamoja na simba atakula majani makavu kama maksai.
8
Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka mwenye sumu kali, naye mtoto mdogo ataweka mkono wake kwenye kiota cha nyoka mwenye sumu.
9
Hawatadhuru wala kuharibu juu ya mlima wangu mtakatifu wote, kwa kuwa dunia itajawa na kumjua BWANA kama maji yajazavyo bahari.
10
Katika siku hiyo, shina la Yese litasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa, mataifa yatamkusanyikia na mahali pake pa kupumzika patatukuka.
11
Katika siku hiyo Bwana atanyosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi na kutoka visiwa vya baharini.
12
Atainua bendera kwa mataifa na kuwakusanya Waisraeli walioko uhamishoni; atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika katika pembe nne za dunia.
13
Wivu wa Efraimu utatoweka na adui wa Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamwonea Yuda wivu wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu.
14
Watawashukia katika mitelemko ya Wafilisti hadi upande wa magharibi, kwa pamoja watawateka watu nyara hadi upande wa mashariki. Watawapiga Edomu na Moabu, na Waamoni watatawaliwa nao.
15
BWANA atakausha ghuba ya Bahari ya Misri; kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake juu ya Mto Eufrati. Ataugawanya katika vijito saba ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.
16
Itakuwepo njia kuu kwa mabaki ya watu wake wale waliosalia kutoka Ashuru, kama ilivyokuwa kwa Israeli walipopanda kutoka Misri.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66