bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Isaiah 19
Isaiah 19
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 20 →
1
Neno kuhusu Misri: Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka naye anakuja Misri. Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake, nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.
2
“Nitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri, ndugu atapigana dhidi ya ndugu, jirani dhidi ya jirani, mji dhidi ya mji, ufalme dhidi ya ufalme.
3
Wamisri watakufa moyo, na nitaifanya mipango yao kuwa batili, watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, kwa wapiga ramli na kwa wale waongeao na mizimu.
4
Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana mkatili na mfalme mkali atatawala juu yao,” asema Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote.
5
Maji ya mito yatakauka, chini ya mto kutakauka kwa jua.
6
Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Mafunjo na nyasi vitanyauka,
7
pia mimea iliyoko kandokando ya Mto Nile, kwenye mdomo wa mto unapomwaga maji baharini. Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Nile litakauka, litapeperushwa na kutoweka kabisa.
8
Wavuvi watalia na kuomboleza, wale wote watupao ndoano katika Mto Nile, watadhoofika kwa majonzi.
9
Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa, wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo.
10
Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa, nao vibarua wataugua moyoni.
11
Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?
12
Wako wapi sasa watu wako wenye hekima? Wao wakuonyeshe na kukufahamisha ni nini BWANA Mwenye Nguvu Zote amepanga dhidi ya Misri.
13
Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu, viongozi wa Memfisi wamedanganyika, walio mawe ya pembe ya taifa lake wameipotosha Misri.
14
BWANA amewamwagia roho ya kizunguzungu; wanaifanya Misri iyumbeyumbe katika yale yote inayoyafanya, kama vile mlevi ayumbayumbavyo katika kutapika kwake.
15
Misri haiwezi kufanya kitu cho chote, cha kichwa wala cha mkia, cha tawi la mtende wala cha unyasi.
16
Katika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa BWANA Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao.
17
Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho BWANA Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.
18
Katika siku hiyo miji mitano ya Misri itazungumza lugha ya Kanaani na kuapa kumtii BWANA Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu.
19
Katika siku hiyo patakuwepo madhabahu ya BWANA katikati ya Misri na mnara wa kumbukumbu kwa BWANA kwenye mpaka wa Misri.
20
Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya BWANA Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia BWANA kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea Mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa.
21
Hivyo BWANA atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali BWANA. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea BWANA nadhiri na kuzitimiza.
22
BWANA ataipiga Misri kwa tauni, atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia BWANA, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya.
23
Katika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja.
24
Katika siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu, pamoja na Misri na Ashuru, nao watakuwa baraka kwa dunia.
25
BWANA Mwenye Nguvu Zote atawabariki, akisema, “Baraka iwe kwa Misri watu wangu, kwa Ashuru kazi ya mikono yangu na kwa Israeli urithi wangu.”
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66