bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Isaiah 36
Isaiah 36
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 37 →
1
Katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwa Mfalme Hezekia, Mfalme Senakeribu wa Ashuru alishambulia miji yote ya Yuda yenye maboma na kuiteka.
2
Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma Amirijeshi kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Amirijeshi aliposimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu lililojengwa, katika njia iendayo kwenye uwanda wa Dobi,
3
Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna aliyekuwa katibu na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wakamwendea.
4
Amirijeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia, “ ‘Hili ndilo asemalo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru: Ni wapi ulikoweka hili tumaini lako?
5
Unasema mnayo mikakati na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Je, wewe unamtegemea nani, hata kwamba unaniasi mimi?
6
Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huutoboa na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea.
7
Kama ukiniambia, “Tunamtumainia BWANA, Mungu wetu,” si ni yeye ambaye mahali pake pa juu na madhabahu zake Hezekia ameziondoa, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima msujudu mbele ya madhabahu hii”?
8
“ ‘Njoni sasa, fanyeni patano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi 2,000, kama wewe unaweza kuwapandisha watu juu yao!
9
Wawezaje basi kurudisha nyuma mmoja wa maafisa wangu wadogo wa bwana wangu, hata kama unaitegemea Misri kwa ajili ya magari ya vita na wapanda farasi?
10
Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza nchi hii bila BWANA? BWANA mwenyewe aliniambia niingie niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’ ”
11
Ndipo Eliakimu, Shebna na Yoa wakamwambia Amirijeshi, “Tafadhali, zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania watu walioko juu ya ukuta wakiwa wanasikia.”
12
Lakini Amirijeshi akajibu, “Kwani ni kwa bwana wenu na ninyi peke yenu ambao bwana wangu amenituma kusema mambo haya, wala si kwa watu walioketi juu ya ukuta, ambao, kama ninyi, itawapasa kula mavi yao na kunywa mkojo wao wenyewe?”
13
Ndipo Amirijeshi akasimama na kuita kwa lugha ya Kiebrania, “Sikilizeni maneno ya mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru!
14
Hili ndilo mfalme asemalo: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa!
15
Msikubali Hezekia awashawishi kumtumaini BWANA wakati anaposema, ‘Hakika BWANA atatuokoa sisi, mji huu hautatiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’
16
“Msimsikilize Hezekia. Hili ndilo mfalme wa Ashuru asemalo: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka katika mzabibu wake na mtini wake mwenyewe na kunywa maji kutoka katika kisima chake mwenyewe,
17
mpaka nije nikawachukue mwende kwenye nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na ya mashamba ya mizabibu.
18
“Msikubali Hezekia awapotoshe wakati asemapo, ‘BWANA atatuokoa.’ Je, mungu wa taifa lo lote ameshawahi kuokoa nchi yake kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru?
19
Wako wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Wako wapi miungu ya Sefarvaimu? Je, wameokoa Samaria kutoka katika mkono wangu?
20
Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya nchi hizi aliyeweza kuokoa nchi yake kutoka kwangu? Inawezekanaje basi BWANA kuiokoa Yerusalemu kutoka katika mkono wangu?”
21
Lakini watu wakakaa kimya wala hawakujibu lo lote, kwa kuwa mfalme aliamuru kuwa, “Msimjibu.”
22
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia kiongozi wa jumba la kifalme, Shebna katibu na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa na kumwambia yale Amirijeshi aliyosema.
← Chapter 35
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 37 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66