bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Matthew 1
Matthew 1
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 2 →
1
Habari za ukoo wa Isa Al-Masihi mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu:
2
Ibrahimu akamzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,
3
Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, Peresi akamzaa Hesroni, Hesroni akamzaa Aramu,
4
Aramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni,
5
Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu, Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu, Obedi akamzaa Yese,
6
Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme. Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.
7
Sulemani akamzaa Rehoboamu, Rehoboamu akamzaa Abiya, Abiya akamzaa Asa,
8
Asa akamzaa Yehoshafati, Yehoshafati akamzaa Yoramu, Yoramu akamzaa Uzia,
9
Uzia akamzaa Yothamu, Yothamu akamzaa Ahazi, Ahazi akamzaa Hezekia,
10
Hezekia akamzaa Manase, Manase akamzaa Amoni, Amoni akamzaa Yosia,
11
wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.
12
Baada ya uhamisho wa Babeli: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli akamzaa Zerubabeli,
13
Zerubabeli akamzaa Abiudi, Abiudi akamzaa Eliakimu, Eliakimu akamzaa Azori,
14
Azori akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Akimu, Akimu akamzaa Eliudi,
15
Eliudi akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Matani, Matani akamzaa Yakobo,
16
naye Yakobo akamzaa Yusufu ambaye alikuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi.
17
Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Al-Masihi.
18
Basi kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho wa Mwenyezi Mungu.
19
Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa, alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, bali aliazimu kumwacha kwa siri.
20
Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mwenyezi Mungu.
21
Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Isa, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”
22
Haya yote yalitukia ili litimie lile Mwenyezi Mungu alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema:
23
“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”
24
Yusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Mwenyezi Mungu, akamchukua Mariamu kuwa mke wake.
25
Lakini hawakukutana kimwili mpaka Mariamu alipojifungua mwanawe kifungua mimba, akamwita Jina lake Isa.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28