bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Matthew 4
Matthew 4
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 5 →
1
Kisha Isa akaongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu kwenda nyikani ili akajaribiwe na ibilisi.
2
Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa.
3
Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4
Lakini Isa akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”
5
Ndipo ibilisi akamchukua Isa mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu,
6
akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika zake, nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”
7
Isa akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mwenyezi Mungu wako.’ ”
8
Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Isa mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake,
9
kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.”
10
Isa akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mwenyezi Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ”
11
Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.
12
Isa aliposikia kwamba Yahya alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya.
13
Akaondoka Nasiri akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali,
14
ili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema:
15
“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kwenye njia ya kuelekea baharini, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya watu wa Mataifa:
16
watu wale waliokaa gizani wameona nuru kuu; nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.”
17
Tangu wakati huo, Isa alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”
18
Isa alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi.
19
Isa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”
20
Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
21
Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Isa akawaita.
22
Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.
23
Isa akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.
24
Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Shamu, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.
25
Makutano makubwa ya watu yakawa yanamjia kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Uyahudi na kutoka ng’ambo ya Mto Yordani.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28