bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Colossians 1
Colossians 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 2 →
1
Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, na ndugu Timoteo
2
tunawaandikia ninyi mlioko Kolose, ndugu watakatifu mnaomtegemea Kristo: Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba yetu!
3
Twamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tunapowaombea ninyi.
4
Kwani tumesikia, mnavyomtegemea Kristo Yesu, tena mnavyowapenda watakatifu wote.
5
Maana mwakishika kingojeo cha yale, mliyowekewa mbinguni; hayo mmeyasikia kale, mlipotangaziwa Utume mwema wa neno la kweli.
6
Nao Utume ulifika kwenu, kama ulivyofika po pote ulimwenguni: huzaa matunda, tena hukua. Vivyo hivyo uko hata kati yenu tangu siku ile, mlipousikia na kuutambua upole wa Mungu kwamba: Ndio wenye kweli.
7
Ndivyo, mlivyofundishwa na Epafura; ni mtumwa mwenzetu mpendwa, tena ni mtumishi mwelekevu wa Kristo anayewafanyizia ninyi kazi.
8
Naye ndiye aliyetueleza, mnavyopendana Rohoni.
9
*Kwa hiyo hata sisi tangu siku ile, tulipoyasikia mambo hayo, hatuachi kumwangukia Mungu na kuwaombea ninyi, mpate kuyatambua yote, ayatakayo, kisha mpewe werevu wote ulio wa kweli na ujuzi wote wa Kiroho.
10
Hivyo mtaweza kuendelea na kumpatia Bwana macheo, apendezwe nanyi kabisa; kisha mtazaa matunda mkizifanya kazi njema zote kwa kuendelea kumtambua Mungu.
11
Tena tunawaombea, mtiwe nguvu zo zote kwa hivyo, utukufu wake ulivyo wenye nguvu, mpate kuyavumilia na kuyanyenyekea yote.
12
Mpate hata kumshukuru Baba kwa furaha, maana amewatengeneza ninyi, mgawiwe fungu la urithi wa watakatifu uliomo mwangani.
13
Yeye ndiye aliyetuokoa katika nguvu ya giza, akatukalisha kwenye ufalme wa mwana wake mpendwa.
14
Mwake yeye ndimo, tupatiamo ukombozi kwa kuondolewa makosa.*
15
Yeye anafanana na Mungu asiyeonekana; ndiye aliyevitangulia viumbe vyote kuzaliwa.
16
Tena ndiye, ambaye vyote viliumbwa mwake yeye, vilivyoko mbinguni navyo vilivyopo nchini, vinavyoonekana navyo visivyoonekana, vikiwa viti vya kifalme au maboma au makao ya wakuu au pengine penye nguvu: vyote pia viliumbwa naye, tena humwelekea.
17
Naye mwenyewe alikuwapo, vitu vyote vilipokuwa havijakuwapo bado, navyo vyote hushikwa naye.
18
Naye mwenyewe ni kichwa cha mwili, maana cha wateule. Naye ni wa kwanza, ni limbuko la wafu, kusudi yeye awe wa kwanza katika mambo yote.
19
Kwani ilimpendeza Mungu, yote pia yamkalie yeye,
20
tena yote yapatanishwe naye, yarudi kwake yeye, kwani hapo, damu yake ilipomwagwa msalabani, ameyapatia utengemano yale yote yaliyopo nchini nayo yaliyopo nchini nayo yaliyoko mbinguni.
21
Hata ninyi kale mlikuwa wageni naye, mkawa hata wachukivu wake, maana mioyoni mlifuata matendo mabaya.
22
Lakini sasa amewapatanisha hata ninyi hapo, alipokufa na kuutoa mwili wake wa kimtu, awageuze nanyi kuwa machoni pake watakatifu pasipo kilema wala kosa.
23
Mtakuwa hivyo mkifuliza kumtegemea, kwani mmajengwa juu ya msingi wenye nguvu, msiwezekane kuondolewa penye kingojeo cha Utume mwema, mliousikia; ndio unaotangaziwa kila kiumbe kilichoko chini ya mbingu. Nami Paulo ninautumikia.
24
Sasa nafurahiwa nayo mateso, niliyoyapata kwa ajili yenu. Nayo maumivu, Kristo aliyoyasaza, nayatimiliza katika mwili wangu, unapoteswa kwa ajili ya mwili wake, maana wateule wake.
25
Ndio wao, niwatumikiao nikiufuata utunzaji wa Mungu, niliopewa, niwatimilizie ninyi Neno lake Mungu.
26
Ni lile fumbo lililokuwa limefichwa tangu kale, baba wasilijue. Lakini sasa watakatifu wake wamekwisha kufumbuliwa;
27
kwani ndio, Mungu aliotaka kuwatambulisha, limbuko likuavyo, lile la utukufu wa fumbo hili, awalimbikialo wamizimu, ndilo hili: Kristo yumo mwenu, yeye ndio utukufu unaongojewa.
28
Naye ndiye, tunayemtangaza sisi, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu werevu wote ulio wa kweli, tupate kumgeuza kila mtu kuwa mtimilifu kwa nguvu ya Kristo.
29
Kazi hii ndiyo, niisumbukiayo na kuishindania kwa uwezo wake yeye anayeniwezesha hivyo kwa nguvu yake.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4