bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Colossians 3
Colossians 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 4 →
1
*Basi, kama mmefufuka pamoja naye Kristo, yatafuteni yaliyoko juu! Ndiko, Kristo akaako kuumeni kwa Mungu.
2
Yawazeni yaliyoko juu, msiyawaze yaliyopo nchini!
3
Kwani mmekufa, lakini uzima wenu uko umefichwa pamoja na Kristo kwake Mungu.
4
Hapo Kristo aliye uzima wenu atakapofunuliwa, ndipo, nanyi mtakapofunuliwa pamoja naye kuwa wenye utukufu.*
5
Basi, viueni viungo viyatimizavyo yaliyopo nchini: ugoni na uchafu na tamaa na kijicho kiovu na choyo kilicho sawa na kutambikia vinyago!
6
Kwa ajili ya mambo hayo makali ya Mungu hutokea.
7
Nanyi mambo hayo mliandamana nayo hapo kale, mlipokuwa mkiyakalia.
8
Lakini sasa nanyi hayo yote sharti myatoke: makali na mifundo ya mioyo na maovu na matusi na mateto mabaya yaliyomo vinywani mwenu.
9
Msiambiane yaliyo ya uwongo! Mvueni mtu wenu wa kale pamoja na matendo yake!
10
Mvaeni yule mtu mpya apataye upya kwamba: Katika utambuzi afanane naye aliyemwumba!
11
Hapo hapana tena Mgriki na Myuda, wala aliyetahiriwa na mwingine asiyetahiriwa, wala mgeni na mshenzi, wala mtumwa na mwungwana. Ila Kristo ndiye yote, naye yumo mwao wote.
12
*Ninyi watakatifu na wapendwa, kwa hivyo, mlivyochaguliwa na Mungu, vaeni mioyo yenye huruma za kweli na utu na unyenyekevu na upole na uvumilivu!
13
Mvumiliane ninyi kwa ninyi na kuachiliana, mtu akiwa na neno la kumkamia mwenziwe! Kama naye Bwana alivyowaachilia ninyi, vivyo hivyo vifanyeni nanyi!
14
Lakini lililo kuu kuliko haya yote: uvaeni upendano! Maana ndio unaoyatimiza yote na kutupatanisha kuwa mmoja.
15
Nao utengemano wa Kristo utawale mioyoni mwenu! Kwani ndio, mlioitiwa, maana m mwili mmoja. Tena mema, mliyogawiwa, myavumishe!
16
Neno la Kristo likae mwenu, kama ni mali, mzikaliazo, mkifundishana pamoja na kuonyana na kujulishana ujuzi wote, mmwimbie Mungu mioyoni mwenu shangwe na nyimbo na tenzi za Kiroho za kwamba: Tumegawiwa mema!
17
Nayo yote, mtakayoyatenda, ikiwa maneno ya kusema au kazi za kufanya, yafanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu mkimvumisha Mungu Baba kwa kufanya hivyo!*
18
Ninyi wake, watiini waume wenu, kama inavyowapasa walio wa Bwana!
19
Ninyi waume, wapendeni wake zenu, msiwaendee kwa ukali!
20
Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote! Kwani hivi vinampendea Bwana.
21
Ninyi baba, msiwachokoze watoto wenu, wasishindwe na kutii!
22
Ninyi watumwa, katika mambo yote watiini walio mabwana zenu kimtu! Msiwatumikie hapo machoni tu, kama wenye kupendeza watu, ila kama wenye kumwogopa Bwana watumikieni kwa mioyo iliyo na neno moja tu!
23
Katika yote, mnayoyatenda, zifanyeni kazi zenu kwa mioyo, kama ni kazi zinazofanyiziwa Bwana, zisizofanyiziwa watu!
24
Jueni, ya kuwa mtapokea kwake Bwana malipo hapo, mtakapoupata urithi wenu! Mtumikieni Bwana Kristo!
25
Lakini mpotovu atayatwaa mapato yao yale, aliyoyapotoa, lakini hakuna upendeleo.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4