bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Colossians 4
Colossians 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
1
Ninyi mabwana, wapeni watumwa wenu yawapasayo, mwalinganishe! Jueni, nanyi mko na Bwana mbinguni!
2
Fulizeni kumwomba Mungu! Kesheni kuomba na kushukuru!
3
Na sisi vilevile tuombeeni, Mungu atufungulie mlango wa kuingizamo Neno lake, tupate kulisema fumbo la Kristo, ni lilelile, nililofungiwa,
4
nipate kulifumbua, kama inavonipasa kulisema!
5
Walioko nje waendeeni kwa werevu wa kweli! Siku mlizopewa, mzitumie vema!
6
Maneno yenu yawe po pote ya kupendeza yakiwa matamu kama yenye chumvi, mpate kujua yanayofaa ya kumjibu mtu awaye yote!
7
Mambo yangu yote yalivyo, atawatambulisha Tikiko aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwelekevu na mtumwa mwenzangu, kwa kuwa wake Bwana.
8
Nami nimemtuma kwenu kwa ajili ya neno lili hili, mpate kuyatambua mambo yetu, naye ataituliza mioyo yenu.
9
Anaye Onesimo, ni ndugu mwelekevu, nimpendaye, ni mtu wa kwenu. Watawatambulisha, yote ya huku yalivyo.
10
Aristarko, mfungwa mwenzangu, na Marko, mpwae Barnaba, wanawasalimu ninyi; kwa ajili yake yeye mmepata maagizo; atakapokuja kwenu, mpokeeni!
11
Naye Yesu anayeitwa Yusto anawasalimu. Kwao Wakristo wa Kiyuda ni hao watatu tu walio wenzangu wa kazi ya kuujenga ufalme wa Mungu, ndio walionituliza moyo.
12
Epafura aliye wa kwenu anawasalimu; ni mtumwa wa Kristo Yesu, naye huwagombea kila siku na kuwaombea, mpate kusimama wenye kuyatimiza na kuyatambua yote, Mungu ayatakayo.
13
Kwani namshuhudia kwamba: Hujisumbua sana kwa ajili yenu na kwa ajili yao walioko Laodikia na Hierapoli.
14
Luka aliye mganga mpendwa na Dema wanawasalimu.
15
Wasalimieni ndugu walioko Laodikia, naye Nimfa nao wateule waliomo nyumbani mwake!
16
Barua hii, ikiisha kusomwa kwenu, angalieni, isomwe hata kwao wateule wa Laodikia, nanyi mwisome ile ya Laodikia!
17
Tena mwambieni Arkipo: Uangalie utumishi wako, ulioupokea wa kumtumikia Bwana, uutimize vema!
18
Salamu hii naiandika kwa mkono wangu mimi Paulo. Ikumbukeni hii minyororo yangu! Upole uwakalie! Amin.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
All chapters:
1
2
3
4