bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Habakkuk 1
Habakkuk 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 2 →
1
Bwana, hata lini nikulilie, unisaidie? Nawe husikii!
2
Hata lini nikulalamikie kwa kukorofishwa? Nawe huniokoi!
3
Mbona umeniacha, nione maovu, ukatazama tu, ninavyosumbuliwa? Uangamizo na ukorofi uko mbele yangu, yako magombano, hata mashindano hutokea.
4
Kwa hiyo Maonyo yanakosa nguvu, mashauri yapasayo hayatokei kale na kale, kwani asiyemcha Mungu humnasa aliye mwongofu, kwa hiyo yanyokayo yakitokea yamekwisha kupotolewa.
5
Yatazameni mambo yaliyoko kwa wamizimu, myaangalie! Ndipo, mtakapozizimka kwa kustuka. Kwani mimi hizi siku zenu nitatenda tendo, kama lingesimuliwa, msingeliitikia.
6
Kwani mtaniona, nikiwainua Wakasidi, lile taifa kali lenye mioyo miepesi, ni wale wanaokwenda katika nchi za mbali, wajipatie makao yasiyo yao.
7
Ndio watu watishao kwa kutia woga, kwao hao hutoka amri zilizo za majivuno tu.
8
Farasi wao hupiga mbio kushinda machui, ni wepesi sana kuliko mbwa wa mwitu wawindao jioni. Wapanda farasi wa kwao hujitata; tena hao wapanda farasi wakija kutoka mbali huruka kama tai wakimbiliao kula.
9
Wao wote hujia kukorofisha, nyuso zao zote pia zikiwa zimeelekea mbele, hukusanya mateka kama ni mchanga.
10
Hao ndio watakaowafyoza wafalme, hata wakuu watawacheka; hao ndio watakaoteka kila boma, maana hulikusanyia mchanga kuwa boma, kisha huliteka.
11
Baadaye hujiendea kama upepo, huenda zao na kuzidi kukosa, nguvu zao huziwazia kuwa mungu wao.
12
Kumbe wewe Bwana, siwe Mungu wangu mtakatifu toka kale? Kwa hiyo hatutakufa. Wewe Bwana, umemweka, atupatilize; wewe Mwamba wetu, umemtia nguvu, atuchapue.
13
Macho yako yanatakata, hayawezi kuyaona tu hayo mabaya, huwezi kabisa kuvitazama tu, watu wanavyosumbuliwa. Mbona sasa unawatazama tu wapokonyaji na kujinyamazia kimya, asiyekucha akimmeza aliye mwongofu kuliko yeye?
14
Unataka, watu wawe kama samaki wa baharini au kama wadudu wakosao awatawalaye?
15
Yeye amewapandisha hawa wote kwa ndoana, akawakamata namo katika nyavu zake, akawakusanya katika majarifa yake, kwa hiyo akafurahi na kupiga vigelegele.
16
Kwa sababu hii huzitambikia nyavu zake, huyavukizia nayo majuya yake, kwani kwa msaada wao mafungu yake ni yenye manono, navyo vyakula vyake ni vyenye mafuta.
17
Je? Kwa hiyo utamwacha, awatoe vivyo hivyo, wavu wake uliowakamata, akiendelea kuua mataifa mazima pasipo kuwahurumia?
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3