bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Habakkuk 3
Habakkuk 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
1
Bwana, nimeusikia utume wako, nikaogopa. Bwana, itokeze kazi yako, iwepo katika miaka ijayo!
2
Ijulishe katika miaka ijayo! Ukikasirika zikumbuke huruma! (Kituo.)
3
Mungu alikuja toka Temani, Mtakatifu alitoka mlimani kwa Parani. Utukufu wake huzifunika mbingu, nchi hii nayo hujaa matukuzo yake.
4
Huangaza kama mwanga wa jua, miali hutoka mkononi mwake; ndimo, nguvu zake zifichikamo.
5
Magonjwa yauayo humtangulia, nazo homa kali huifuata miguu yake.
6
Anaposimama ndipo, anapoitetemesha nchi; anapochungulia ndipo, anapoyastusha mataifa. Milima iliyoko toka kale huatuka, vilima vilivyoko kale na kale huangukiana chini; ni vilevile, alivyovikanyaga juu tangu kale alipopita.
7
Vijumba vya Wanubi niliviona vyenye shida, nayo mahema ya nchi ya Midiani yakatikisika.
8
Je? Bwana anaikasirikia mito? Makali yako yataitokea mito? Je? Machafuko yako yanaiendea bahari? Kwa kuwa unavutwa na farasi katika gari lako lishindalo!
9
Uta wako umefunuliwa, utokee waziwazi, kama ulivyoziapia koo za watu kwa neno lako (Kituo.) Unapoipasua nchi, hapo hutokea majito.
10
Ukioneka, milima hustuka, nayo mafuriko ya maji huzidi, vilindi vya baharini huvuma na kuikweza mikono yao juu.
11
Jua na mwezi husimama kwao, mishale yako ikija kumulika, nao umeme wa mkuki wako ukimetameta.
12
Kwa kukasirika unaikanyaga nchi, kwa kuchafuka unayaponda mataifa.
13
Umetokea kuwaokoa walio ukoo wako, upate kumwokoa uliyempaka mafuta, ukaviponda vichwa vyao wasiokucha nyumbani mwao, ukazibomoa toka misingi hata vipaani. (kituo.)
14
Kwa mikuki yao unavichoma vichwa vya vikosi vyao vijavyo mbio kama kimbunga kunikimbiza mimi na kunizomea kama watu wanaotaka kula mnyonge fichoni pake.
15
Lakini wewe ukaja na kuikanyaga bahari ukipanda farasi wako, ijapo maji mengi yavume.
16
Nilipoyasikia, ndipo, tumbo langu lilipotetemeka, midomo yangu nayo ikajipigapiga kwa uvumi wao, ugonjwa wa ubovu ukaingia mifupani mwangu, nikatetemeka wote hata chini, niliposimama, kwa sababu sina budi kuingoja siku ya kusongwa, itakapolipata lile kabila lililokuja kutushambulia.
17
Kwani mkuyu hauchanui, wala mizabibu haizai, vichipukizi vya mchekele navyo hudanganya, mashamba ya ngano hayaleti chakula, kondoo wametoweka mazizini kwao, hata ng'ombe hamna vibandani mwao.
18
Lakini mimi ninayemfurahia, ndiye Bwana, ninamshangilia Mungu wangu aliyeniokoa.
19
Bwana Mungu ndiye aliye nguvu yangu! Anipa miguu ipigayo mbio kama yake kulungu, akiniendesha vema, nifike juu vilimani kwangu. Kwa mwimbishaji, ayaimbie mazeze yangu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
All chapters:
1
2
3