bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Habakkuk 2
Habakkuk 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
1
Na nije kusimama pangu pa kulindia, ningoje zamu mnarani juu! Na nichungulie, nione, atakayoniambia, niyajue, nitakayoyajibu kwa ajili ya malalamiko yangu.
2
Bwana akaniitikia, akaniambia: Liandike, uliloliona, ulichore katika vibao, watu wapate kulisoma mumo humo upesi.
3
Kwani hilo ono liko na siku zake, hazijatimia bado, lakini linajihimiza kumalizika, haliongopi. Ingawa likawie, lingojee! Kwani halina budi kuja, halitachelewa.
4
Utaona, moyo wake umejitutumua wenyewe, haunyoki; lakini mwongofu atapata uzima kwa kumtegemea Mungu.
5
Kweli mvinyo hudanganya: mtu mwenye majivuno hawezi kutulia, ingawa aupanue moyo wake kuwa kama kuzimu, ingawa awe kama kifo, hawezi kushiba, sharti akusanye kwake mataifa yote, kweli sharti ayapeleke kwake makabila yote ya watu.
6
Je? Hao wote hawatamtungia mafumbo ya kumsimanga na kumfyoza kwamba: Yatampata achukuaye mengi yasiyo yake! Ataviweza mpaka lini? Hata mizigo mizima ya mali, wengine walizompa, awawekee, amejipa, ziwe zake.
7
Je? Hawatainuka kwa mara moja, wakuumize? Hawataamka, wakusumbue? Ndipo, utakapotekwa nao!
8
Kwa kuwa wewe ulipokonya mali za mataifa mengi, kwa hiyo wao wa masao ya makabila yote watazipokonya mali zako, wazilipize damu ya watu, ulizozimwaga, wakulipishe nayo makorofi, ambayo uliitendea nchi na miji na wenyeji wao wote.
9
Yatampata aupatiaye mlango wake mapato mabaya, apate kujitengenezea kiota juu kwamba: ajiepushe mikononi mwao wabaya.
10
Mashauri yako yatautia mlango wako soni: ulipoangamiza makabila mengi, umeikosesha roho yako.
11
Kwani majiwe yaliyomo ukutani yatapiga kelele, nayo miti ya kipaga itaitikia.
12
Yatampata ajengaye miji kwa damu na kuishupaza mitaa yake kwa mapotovu!
13
Je? Hamjayaona yatokayo kwake Bwana Mwenye vikosi? Namwone: Makabila ya watu waliyoyasumbukia, huliwa na moto, nayo, mataifa waliyoyafanyia kazi na kujichokesha, huwa ya bure.
14
Kwani nchi hii itajazwa nao waujuao utukufu wa Bwana, kama maji yanavyofurikia baharini na kuyafunika yote
15
Yatampata amnyweshaye mwenziwe kinywaji, alichokichanganya na makali yake! Kisha anamlewesha, kusudi auone uchi wake na kumfurahia!
16
Umejishibisha yatiayo soni ukiyaacha yenye utukufu, lakini wewe nawe sharti unywe, ujulikane kuwa mtu asiyetahiriwa. Kikombe kilichomo kuumeni mwa Bwana kinakufikia, utukufu wako ufunikwe nayo yenye soni.
17
Kwani makorofi, ambayo uliitendea Libanoni, yatakufunika, nao nyama, uliowaua bure tu, watakutia woga, kwa ajili ya damu za watu, ulizozimwaga kwa kuikorofisha nchi na miji pamoja na wenyeji wao wote.
18
Hapo kinyago kilichochongwa kitafaaje? Maana ni kazi tu ya fundi aliyekichonga. Au kinyago cha vyuma vilivyoyeyushwa kifundishacho uwongo tu kitafaaje? Maana ni egemeo lake fundi aliyekitengeneza, apate miungu isiyosema.
19
Yatampata akiambiaye kipande cha mti: Amka! naye akiambiaye kipande cha jiwe lisilosema: Inuka! Je? Hicho kitaweza kufumbua neno? Kitazame! Kimefunikwa na dhahabu na fedha, lakini ndani yake hamna pumzi yo yote.
20
Lakini Bwana yumo Jumbani mwake mwenye utakatifu, usoni pake kila mtu wa nchi hii anyamaze kimya!
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3