bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Nahum 1
Nahum 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 2 →
1
Hili ndilo tamko zito la kuuambia Niniwe yatakayoupata, ni kitabu cha maono, Nahumu wa Elkosi aliyoyaona.
2
Bwana ni Mungu mwenye wivu alipizaye; kwani Bwana ni mlipizaji mwenye makali, Bwana huwalipiza wapingani wake, nao wachukivu wake huwashikia makali.
3
Bwana ni mvumilivu, mwenye nguvu kuu, lakini aliye mkosaji hamwachilii, asimpatilize. Njia yake Bwana imo katika kimbunga na katika upepo mkali, nayo mawingu ndiyo mavumbi ya miguu yake.
4
Akiikaripia bahari, anaipwelesha, nayo mito mikubwa yote anaikausha. Nchi za Basani na za Karmeli zimezimia, nayo majani na maua ya Libanoni yamezimia.
5
Milima hutetemeka mbele yake, navyo vilima hutikisika; nayo nchi huinukia usoni pake pamoja na ulimwengu nao wote wakaamo.
6
Yuko nani awezaye kusimama, akimkasirikia? Au yuko nani awezaye kukaa katika makali yake yenye moto? Hasira yake ichomayo humwagika kama moto wenyewe, nayo miamba hupasuliwa nayo.
7
Bwana ni mwema, ni ngome siku ya masongano, huwajua wamkimbiliao.
8
Lakini kwa mafuriko ya maji yatosayo atapamaliza mahali pao wengine, nao wachukivu wake atawakimbiza gizani.
9
Mwawaziaje kumpingia Bwana? Yeye ndiye atakayewamaliza, masongano yasitokee mara ya pili.
10
Ingawa washikamane kama miiba iliyosukwa, au ingawa waloe kwa mvinyo, wawe majimaji kama mvinyo zao, wote pia wataliwa na moto kama majani makavu.
11
Mwako wewe ametoka awazaye mabaya ya kumpinga Bwana kwa mashauri maovu, aliyoyatoa.
12
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ingawa wakae na kutulia kwa kuwa wengi hivyo, watakatwa, watoweke. Lakini wewe, kama nimekunyenyekeza, sitakunyenyekeza tena.
13
Sasa nitayavunja makongwa yao, yakuondokee, nayo mafungo uliyofungwa nitayararua.
14
Lakini kwa ajili yako (Asuri) Bwana ameagiza, wenye jina lako wasipewe tena kuzaa, namo nyumbani mwa mungu wako nitavitowesha vinyago vya kuchonga navyo vya kuyeyusha, nawe nitakuchimbia kaburi lako, kwani umeonekana kuwa mwepesi zaidi.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3