bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Nahum 2
Nahum 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
1
Tazameni! Milimani juu iko miguu ya mpiga mbiu atangazaye utengemano: Uzile sikukuu zako, Yuda! Vilipe viapo vyako! Kwani yule mwovu asiyefaa hatapita tena kwako, amekwisha kung'olewa wote pia.
2
Amepanda mwenye kutawanya, akujie; kwa hiyo lilinde boma na kuiangalia njia! Jifunge sana viuno vyako! Nazo nguvu, ulizo nazo, zikaze kabisa!
3
Kwani Bwana anaurudisha utukufu wake Yakobo nao utukufu wake Isiraeli, kwani wapokonyi waliyapokonya yaliyokuwako, nayo matawi ya mizabibu yao waliyaharibu.
4
Ngao za mafundi wake wa vita ni nyekundu, watu wake wenye nguvu wanavaa nguo nyekundu za kifalme, siku, yanapopangwa, vyuma vya magari yake humetuka kama moto, nayo mikuki yake hutikiswatikiswa.
5
Barabarani magari yanapiga vishindo vya nguvu, namo uwanjani yanashindana mbio; mkiyatazama huwa kama mienge ya moto, tena hurukaruka upesi kama umeme.
6
Basi, anawakumbuka wakuu wake, lakini wanakuja na kujikwaakwaa; walipokwenda mbiombio kuufikia ukuta wa boma la nje, kikingio cha kuubomolea kilikuwa kimekwisha kuwekwa.
7
Malango ya upande wa mtoni yalipofunguliwa, waliomo jumbani mwa mfalme wakayeyuka.
8
Mke wa mfalme hana budi kuvuliwa nguo na kupelekwa mbali, vijakazi wake wakilia kama sauti za hua na kujipigapiga vifua.
9
Niniwe ulikuwa kama ziwa la maji tangu kale, lakini sasa hao wengi wanajikimbilia tu; wanaambiwa: Simameni! Simameni! Lakini hakuna anayegeuka.
10
Tekeni fedha! Tekeni dhahabu! Kwani malimbiko hayana mwisho; viko vyombo vya kila namna vipendezavyo.
11
Lakini kwa kuwa mioyo imeyeyuka, uko uchi na utupu na ukiwa, nayo magoti yanagotanagotana, viuno vyote vinatetemeka, nazo nyuso zao wote zimewapoa.
12
Makao ya simba yako wapi? Malisho ya wana wa simba yako wapi nayo? Ndipo wapi, walipotembea simba mume na mke na watoto pasipo kuona awastushaye?
13
Ndipo wapi, simba waliporarua nyama, mpaka watoto wao washibe? Ndipo wapi, walipoona nyama wa kuwapatia nao wake zao? Ndipo wapi, walipojaza mapango yao nyama, waliowararua? Yako wapi mashimo yao nyama wao hao, waliowararua?
14
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Utaniona, nikikujia, niyachome magari yako, yawe moshi, nao wana wako wa simba upanga utawala; nitakukomesha, usirarue tena nyama katika nchi, wala sauti za wajumbe wako zisisikilike tena.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3