bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Nahum 3
Nahum 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
1
Yataupata huo mji wenye damu! Wote mzima umejaa uwongo na ukorofi! Haukuacha kupokonya.
2
Na wasikie uvumi wa mijeledi na vishindo vya magurudumu yatutumuayo na vya farasi wapigao mbio na vya magari yarukayo!
3
Wapandao farasi watakuja mbiombio wenye panga ziwakazo moto na wenye mikuki imerimetayo kama umeme. Ndipo, watakapouawa wengi, mizoga iwe chungu zima, watu wakwazwe na mizoga.
4
Hayo ndiyo malipo ya uzinzi mwingi wa huyo mzinzi mke aliye mzuri wa kupendeza, aliyenasa kwa uganga wake, aliyeteka makabila mazima kwa uzinzi wake na milango ya watu kwa uganga wake.
5
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Utaniona, nikikujia, nizifunue nguo zako ndefu nikizipandisha mpaka usoni kwako, nionyeshe mataifa uchi wako, nao walio wa kifalme niwaonyeshe yako yenye soni.
6
Nitakutupia yatapishayo, nikutie soni; nitakuweka kuwa kitisho chao watakaokutazama.
7
Ndipo, kila atakayekuona atapokukimbia na kusema: Kumbe Niniwe umebomolewa! Yuko nani atakayeombolezea? Nitatafuta wapi watakaokutuliza moyo?
8
Je? U mwema kuliko No wa Amoni uliokaa majitoni huko Misri, uliozungukwa na maji? Boma lake ulikuwa wingi wa maji, nao ukuta wa nje wa boma ulikuwa wingi wa maji.
9
Ulipata nguvu kule kwa Wanubi nako kwa Wamisri wasiohesabika, Waputi na Walubi walikuwa tayari kuusaidia.
10
Nao umetekwa na kuhamishwa utumwani, nao watoto wake wachanga wakapondwa vichwa po pote pembeni barabarani; waliokuwa wenye utukufu wakapigiwa kura, nao wakuu wake wote wakafungwa minyororo.
11
Wewe nawe na uleweshwe, uwe kama mtu azimiaye roho, wewe nawe na ujitafutie ngome ya kukimbilia adui.
12
Maboma yako yote inafanana na mikuyu yenye kuyu za kwanza, mtu akiitikisa, zitaangukia kinywani mwake anayetaka kuzila.
13
Waume wako, ulio nao mwako, utawaona kuwa kama wanawake, nayo malango ya nchi yako yatakuwa yamefunguka, yawe wazi mbele ya adui zako, nao moto utayala makomeo yako.
14
Jichotee maji kuwa nayo siku za kusongwa, kayatengeneze maboma yako, yapate nguvu! Ukiisha kuuponda mchanga, ukanyage udongo, nayo tanuru ya kuchomea matofali itengeneze, ipate nguvu!
15
Lakini patakapotimia, moto utakula, nazo panga zitakuangamiza zikikula kama funutu, ingawa mwe wengi kama funutu, ingawa mwe wengi kama nzige.
16
Wachuuzi wako walikuwa wengi kuliko nyota za mbinguni, wakawa kama funutu: wakigeuka kuwa nzige, huruka kwenda zao.
17
Wakuu wako wa serikali wanafanana na nzige, nao wakuu wako wa askari wanafanana na makundi ya nyenze: siku za baridi huja kulala kutani, lakini jua likitoka, hujiendea kwa kuruka, tena mahali, walipokwenda, hapajulikani.
18
Wachungaji wako, mfalme wa Asuri, wamelala, watukufu wako wamelala usingizi. Watu wako wametawanyika milimani juu, tena hakuna anayewakusanya.
19
Donda lako haliwezekani, pigo lililokupiga haliponi kabisa. Wote wazisikiao habari zako watakupigia makofi, kwani yuko nani, ambaye ubaya wako haukumpata siku zote?
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
All chapters:
1
2
3