bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Leviticus 2
Leviticus 2
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 3 →
1
Mutu yeyote akileta sadaka ya ngano kwa Yawe, sadaka hiyo ikuwe ya unga laini. Atautia mafuta na ubani.
2
Kisha, atawaletea hao makuhani, wazao wa Haruni. Atatwaa mukono mumoja wa unga huo laini wenye mafuta na ubani na kumupelekea kuhani mumoja ambaye atauteketeza juu ya mazabahu ukuwe sadaka ya ukumbusho kwa Yawe. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.
3
Sehemu inayobaki ya sadaka hiyo ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.
4
Kama mutu anamutolea Mungu sadaka ya ngano iliyochomwa kwenye furu, hiyo itakuwa ya mikate isiyotiwa chachu ya unga laini uliochanganywa na mafuta ya zeituni, au ya mikate myembamba isiyokuwa na chachu na isiyopakwa mafuta.
5
Ikiwa sadaka unayotoa ni ya mukate uliokaangwa kwenye kikaango, hiyo itakuwa ya unga laini uliochanganywa na mafuta ya zeituni lakini bila chachu.
6
Mikate hiyo itakatwakatwa na kumiminiwa mafuta. Hiyo ni sadaka ya ngano.
7
Kama sadaka unayotoa ni ya mikate iliyopikwa katika sufuria, hiyo itakuwa ya unga laini na imetiwa mafuta.
8
Utaleta sadaka ya ngano iliyotengenezwa kwa vitu hivyo mbele ya Yawe na kuhani ataipeleka kwenye mazabahu.
9
Kuhani atatwaa sehemu ya sadaka hiyo ikiwa ni sadaka ya ukumbusho na kuiteketeza juu ya mazabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.
10
Sehemu inayobaki ya sadaka ya ngano, ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka inayotolewa Yawe kwa moto.
11
Sadaka yoyote ya ngano utakayomuletea Yawe inapaswa kuwa imetengenezwa bila chachu, maana hakuna ruhusa hata kidogo ya kutumia chachu wala asali katika sadaka Yawe anazotolewa kwa moto.
12
Unaweza kumuletea Yawe mazao yako ya kwanza kama sadaka. Lakini hayo hayatatolewa kwenye mazabahu kama harufu ya kumupendeza.
13
Utakoleza sadaka zako zote za ngano kwa chumvi. Usiache hata kidogo kuweka chumvi katika sadaka yako ya ngano, maana chumvi ni kitambulisho cha agano Mungu alilofanya pamoja nanyi.
14
Ukimutolea Yawe sadaka ya mazao yako ya kwanza utaitoa hiyo ikiwa imechomwa katika masuke yake, au utaitoa katika mikate ya kuchomwa iliyotengenezwa kwa ngano iliyosagwa.
15
Utaitia mafuta na kuweka ubani. Hiyo ni sadaka ya ngano.
16
Kuhani atateketeza sehemu ya sadaka hiyo ya ngano iliyopondwa na mafuta pamoja na ubani wake wote, ikuwe sadaka ya ukumbusho. Hiyo ni sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27