bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Romans 14
Romans 14
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 15 →
1
LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake.
2
Mtu mmoja ana imani, anakula vyote, lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
3
Yeye alae asimdharau yeye asiyekula, nae asiyekula asimhukumu yeye alae; kwa maana Mungu amemkubali.
4
Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha.
5
Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawa sawa. Killa mtu athuhutike katika akili zake mwenyewe.
6
Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.
7
Kwa sababu hapana mtu miongoni mwenu aishiye kwa nafsi yake, wala hapana afae kwa nafsi yake.
8
Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Bassi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
9
Maana Kristo alikufa akafufuka akawa hayi tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hayi pia.
10
Lakini wewe je! mbona wamhukumu ndugu yako? na wewe je! mbona wamdbarau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.
11
Kwa maana imeandikwa, Kwa uhayi wangu, anena Bwana, magoti yote yatapigwa mbele zangu, Na ndimi zote zitamkiri Mungu.
12
Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu.
13
Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha.
14
Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najis asili yake, lakini kwake huyu akionae kitu kuwa najis, kwake huyo kitu kile ni najis.
15
Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambae Kristo alikufa kwa ajili yake.
16
Bassi, usitajwe vibaya kwa huo wema wenu.
17
Maana ufalme wa Muugu si kula na kunywa, bali baki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
18
Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo haya humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wana Adamu.
19
Bassi kama ni hivyo, tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.
20
Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Vyote ni safi; bali ni vibaya mtu kula akajikwaza.
21
Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno ambalo ndugu yako hukwazwa au kuangushwa au kuwa dhaifu.
22
Je! unayo imani? Uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Yu kheri mtu yule asiyejihukumu katika neno lile alikubalilo.
23
Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa, kwa maana hakula kwa imani. Na killa tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16